

Lugha Nyingine
Kamanda wa RSF akubali kuondoka katika mji mkuu wa Sudan
(CRI Online) Machi 31, 2025
Kamanda wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) nchini Sudan, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo amekiri kuwa vikosi vyake vimeondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum, akiielezea hatua hiyo kuwa ni ya kimkakati na kuhamia Omdurman, mji mwingine ulio pembezoni mwa mji huo mkuu.
Katika ujumbe wa sauti uliotolewa na Kamanda huyo katika mtandao wa kijamii wa Telegram jana Jumapili, ameviambia vikosi vyake kwamba hatua hiyo imeidhinishwa na kamandi ya usimamizi na operesheni, na kuongeza kuwa vita vya karibu miaka miwili dhidi ya jeshi la Sudan bado viko katika hatua za mwanzo.
Kauli hiyo imeashiria majibu ya kwanza ya moja kwa moja juu ya madai ya Jeshi la Sudan kukomboa maeneo muhimu ya mjini Khartoum, ikiwemo ikulu na majengo ya serikali kuu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma