Simulizi za Msanii wa DRC na Jingdezhen, "Mji Mkuu wa Vyombo vya Udongo wa Milenia" wa China: kama ndege mhamaji wa sanaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2025

Msanii wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mwanga Stanis akichora mchoro wa sahani ya ya udongo. (Picha imetolewa na mhojiwa)

Msanii wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mwanga Stanis akichora mchoro wa sahani ya udongo. (Picha imetolewa na mhojiwa)

Katika Karakana ya Kimataifa ya Sanaa ya Kauri (vyombo vya udongo) ya Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen, Mkoa wa Jiangxi wa China, msanii wa kauri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mwanga Stanis, yuko kimya turi akichora michoro ya sahani za kauri.

"Kila mwaka huwa ninakuwa Jingdezhen kwa wiki chache, kusikiliza mihadhara, kutembelea maonyesho na kubadilishana maarifa na kujifunza na wasanii wa kauri kutoka nchi mbalimbali," anasema Stanis. "Ninatumaini kujifunza zaidi na kufundisha yale niliyojifunza kwa wanafunzi wangu barani Afrika."

Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, Stanis amekuwa akisafiri kwenda na kurudi kati ya Kinshasa na Jingdezhen, kama ndege mhamaji, akivuka umbali wa zaidi ya kilomita 10,000, akiunganisha mabadilishano ya kitamaduni ya kauri ya China na Afrika.

Mwaka 2013, Stanis alifika Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen kusomea shahada ya uzamili katika usanifu wa kauri. Alipofika kwa mara ya kwanza, karakana nyingi za ufinyanzi zilizopo mitaani, na harufu ya udongo wa kauri iliyotapakaa hewani, vilimfanya ahisi kama alikuwa katika jumba la makumbusho ya kauri.

Katika muda wake wa mapumziko, Stanis alipenda kutembelea Soko la Ubunifu la Taoxichuan ili kuzungumza na mafundi wa kauri, na alikuwa akienda katika mitaa na vichochoro vya kale vya Eneo la Kihistoria na Kitamaduni la Taoyangli kushuhudia tanuru za kuni zikifunguliwa.

Kauri ni kitambulisho muhimu cha ustaarabu wa China. Katika miaka ya hivi karibuni, Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen, kama taasisi kiongozi, kilianzisha Shirikisho la Kimataifa la Elimu ya Kauri la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya vyuo na zaidi ya vyuo vikuu 50 kutoka Ulaya, Afrika, na maeneo mengine na kimefundisha zaidi ya wanafunzi wa kigeni 3,000, Stanis akiwa ni mmoja wao.

Msanii wa DRC Mwanga Stanis akibadilishana maarifa ya ubunifu na wasanii kwenye karakana ya kimataifa ya kauri ya Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen, China. (Picha imetolewa na mhojiwa)

Msanii wa DRC Mwanga Stanis akibadilishana maarifa ya ubunifu na wasanii kwenye karakana ya kimataifa ya kauri ya Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen, China. (Picha imetolewa na mhojiwa)

Baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen, Stanis alirejea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kufundisha katika Akademia ya Sanaa za Ufundi cha Kinshasa. Madarasa yake yamejaa majaribio za tamaduni mbalimbali, zikiwawezesha wanafunzi zaidi wa Afrika kuelewa jinsi ya kuchora michoro ya kauri kwa mtindo wa uchoraji wa wino wa Kichina.

"Wakati mwanafunzi walipotumia kwa mara ya kwanza mbinu ya 'kugawanya maji' kuchora mwanga wa asubuhi wa Mto wa Kongo, niliona mwanga kwenye macho yao," anasema Stanis.

Mwaka 2023, Stanis, ambaye kwa sasa ni profesa mshiriki wa Akademia ya Sanaa za Ufundi ya Kinshasa, alirejea tena Jingdezhen. Wakati huu, siyo tu ameanzisha karakana, bali pia amerudi katika chuo chake kilichomfunza, Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen, kufundisha.

"Ninatumaini kuwa wanafunzi wengi zaidi wa Afrika wataweza kuhisi mvuto wa utamaduni wa kauri wa China, kupanua kila mara mbinu elezi za uchoraji wa kauri, na kupata miitiko kati ya tamaduni za Kichina na Kiafrika," anasema Stanis.

(Jina ya mhojiwa limetafsiriwa kwa namna linavyotamkwa.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha