

Lugha Nyingine
Viongozi wa biashara wa nchi za kigeni wasisitiza tena China kama oasisi ya uhakika
BEIJING - Katika Dunia yenye hali ya kuongezeka kwa kujihami kiuchumi, China inaendelea kupanua ufunguaji mlango, ikiingiza utulivu kwenye uchumi wa dunia, na imekuwa oasisi ya uhakika na mahali panapopendwa zaidi kwa uwekezaji na ujasiriamali, hii ni imani inayochangiwa na wawakilishi zaidi ya 40 wa wadao wa wafanyabiashara wa kimataifa waliokutana mjini Beijing siku ya Ijumaa na Rais wa China Xi Jinping.
Kuanzia Baraza la Maendeleo la China Mwaka 2025 mjini Beijing hadi Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Asia la Boao2025 Mkoani Hainan, kusini mwa China, wakurugenzi watendaji hao wa kigeni wamesisitiza dhamira yao kwa China kama soko kuu la uwekezaji na ushirikiano.
Wamesema kuwa, China ina mfumo kamili wa viwanda, mazingira mengi ya matumizi, kiwango kikubwa cha soko na kundi kubwa la vipaji, ambavyo vinachanganyikana kutoa fursa nyingi za ushirikiano kwa uvumbuzi wa kimataifa wa kiviwanda na kiteknolojia.
Washiriki wakihudhuria Baraza la Maendeleo la China 2025 mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 23, 2025. (Xinhua/Li Xin)
Kuwekeza China, Kuwekeza katika siku za baadaye
"Tumekuwa tukijivunia sana kutoa mchango katika maendeleo ya China, kuwezesha na kuunganisha China na dunia," amesema Sean Stein, Mkuu wa Baraza la Biashara la Marekani na China, akiongeza kuwa China imekua hadi kuwa soko la pili kwa ukubwa duniani la soko la walaji, likitoa fursa kubwa kwa kampuni za kimataifa kuwekeza na kupanua biashara zao.
"Tumekuwa zaidi ya miaka 30 sasa nchini China, na tuna vituo kadhaa vya uzalishaji. Kwa upande wetu, ni soko kubwa sana. China pia ni soko la kuvutia sana na yenye fursa nyingi leo, siku za nyuma, lakini pia katika siku zijazo - na ndiyo sababu tuko hapa," amesema Christian Hartel, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Wacker Chemie AG.
Wafanyabiashara wakitembelea eneo la "Wekeza nchini China" la Maonesho ya 24 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China mjini Xiamen, Mkoani Fujian, kusini mashariki mwa China, Septemba 8, 2024. (Xinhua/Lin Shanchuan)
Macho yote kwa nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora
Uwekezaji wa kigeni una jukumu kubwa katika kukuza na kuhimiza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, na China inaunga mkono ushiriki wa kampuni za kigeni katika maendeleo yake mapya ya viwanda, kwa kujikita katika sekta za teknolojia ya hali ya juu, kwa mujibu wa mpango kazi wa kuleta utulivu wa uwekezaji wa kigeni mwaka 2025, ambao uliidhinishwa na mkutano wa utendaji wa Baraza la Serikali la China mwezi Februari.
Msisitizo wa China juu ya uvumbuzi kama kichocheo cha ukuaji wenye sifa bora umewagusa sana wawakilishi wa kibiashara za kigeni. Wamesema kutoka "Made in China" hadi "nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora," China imewezesha mageuzi na uboreshaji wa viwanda kupitia uvumbuzi, na iko katika mazingira mazuri ya kufikia maendeleo yenye sifa bora zaidi na endelevu zaidi.
Wawakilishi hao wa kibiashara wa nchi za kigeni wamefikia maafikiano kwamba mtazamo wa uchumi wa China ni imara.
"Leo kuna dalili nyingi za matumaini katika uwekezaji," Jean-Pascal Tricoire, mwenyekiti wa Schneider Electric amesema.
Picha hii iliyopigwa Novemba 9, 2024 ikionyesha banda la Schneider Electric kwenye Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China mjini Shanghai, mashariki mwa China. (Xinhua/Wang Xiang)
Gari linalotumia umeme la Mercedes-Benz G-Class likionekana pichani kwenye hafla ya uzinduzi katika Maonyesho ya Kimataifa ya Magari ya Beijing Mwaka 2024 mjini Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 25, 2024. (Xinhua/Cai Yang)
Fungua ushirikiano kwa mustakabali wa pamoja wa siku za baadaye
Kutokana na hali ya kuongezeka kwa hali ya upande mmoja na kujihami katika uchumi wa dunia, China imeapa kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, huku ikidumisha utulivu katika biashara na uwekezaji wa kigeni.
China ni oasisi ya uhakika, Kwa mujibu wa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Aramco Amin H. Nasser. "Tunachokiona leo katika mazingira ya kimataifa ni hali ya kutokuwa na uhakika. Tunaona kutotabirika, na tunahitaji utulivu, uhakika na kutabirika kwa China ambako tunauona," Nasser ameeleza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma