

Lugha Nyingine
Mkutano wa "Ubunifu wa Pamoja wa Binadamu na Mashine: Kuwezesha Nguvu Chanya za Ubunifu wa AI 2025" wafanyika Nanning, China
Mkutano wa "Ubunifu wa Pamoja wa Binadamu na Mashine: Kuwezesha Nguvu Chanya za Ubunifu wa AI 2025" ukifanyika usiku wa Machi 29 mjini Nanning, China. (Picha na He Xueqiao na Liang Kaichang)
Ukiwa moja kati ya matukio makuu ya Jukwaa la Vyombo vya Habari vya Mtandaoni la China 2025, "Mkutano wa Ubunifu wa Pamoja wa Binadamu na Mashine: Kuwezesha Nguvu Chanya za Ubunifu wa AI 2025" umefanyika usiku wa Machi 29 mjini Nanning, China.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Uenezi ya Kamati ya Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Zhuang Rongwen, katibu wa kamati ya CPC ya Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, Chen Gang na wageni wengine wa heshima kwa pamoja wamezindua “Mpango wa Ubunifu wenye nguvu chanya wa AI 2025".
Mkutano huo umejikita katika “AI kuwezesha mawasiliano mazuri ya mtandaoni”, na uliwaalika wawakilishi kutoka vyombo vya habari vya mtandaoni, kampuni za mtandao wa intaneti na taasisi za kitafiti ili kubadilishana maoni na kufunzana uzoefu.
Mkutano huo umetangaza matokeo ya shughuli ya Kukusanya na Kuonesha Mifano bora ya ubunifu wa AI wa Mawasiliano ya Mtandaoni ya China 2024. Kazi za “Bendera ya Taifa imepepea kwa miaka 75! AI yaonesha safari ya mshika bendera wa kwanza”, “Confucius anapokutana na Socrates” na “Usiku wa Kuvutia wa AI” na mifano mingine bora imeoneshwa na kuelezwa na wabunifu wao papo hapo.
Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Idara ya Mawasiliano ya Mtandaoni ya Ofisi ya Kamati ya Mambo ya Mtandao wa Intaneti ya Kamati Kuu ya CPC, na Idara ya Usimamizi wa Teknolojia za Mtandao ya ofisi hiyo. Umefanywa kwa pamoja na tovuti ya Gazeti la Umma, na Ofisi ya kamati ya mambo ya Mtandao wa Intaneti ya kamati ya chama ya Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, ukiratibiwa na kampuni ya Video ya Umma, na kuungwa mkono kwa pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Mtandaoni ya China na Mfuko wa Maendeleo ya Mtandao wa Intaneti wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma