Afghanistan na Marekani zajadili kufunguliwa tena kwa ubalozi wa Marekani mjini Kabul

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2025

Picha hii iliyopigwa Machi 27, 2025 ikionyesha Ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Kabul, Afghanistan. (Picha na Saifurahman Safi/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Machi 27, 2025 ikionyesha Ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Kabul, Afghanistan. (Picha na Saifurahman Safi/Xinhua)

KABUL - Msemaji wa serikali ya mpito ya Afghanistan, Zabihullah Mujahid, amesema masuala kadhaa, yakiwemo ya kufunguliwa tena kwa Ubalozi wa Marekani mjini Kabul na kukabidhi mamlaka ya udhibiti wa Ubalozi wa Afghanistan mjini Washington, yamejadiliwa huko Kabul na ujumbe wa Marekani.

"Majadiliano ya kukabidhi Ubalozi wa Afghanistan nchini Marekani yanaendelea," Mujahid amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al Arabiya. "Pia tunataka Ubalozi wa Marekani uanze shughuli zake." amefafanua.

Ujumbe huo ulirejea Marekani na masuala kadhaa, na "tutasubiri kuona ni hatua gani Washington itachukua," Mujahid ameongeza.

Amesema kuwa serikali ya mpito ya nchi hiyo imekomesha vita na Marekani na ina dhamira ya kuanzisha uhusiano wa kuhimiza hamasa na nchi hiyo.

Tangu serikali hiyo ya mpito kuchukua mamlaka Agosti 2021, ujumbe wa Marekani ulitembelea Kabul wiki iliyopita kwa mara ya kwanza.

Ujumbe huo ulifanya majadiliano na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya mpito ya Afghanistan, Mawlawi Amir Khan Muttaqi kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala ya kubadilishana wafungwa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha