The Atlantic lachapisha jumbe zote za mazungumzo ya kundi la viongozi waandamizi wa Marekani kuhusu mashambulizi dhidi ya Yemen

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2025

Picha iliyopigwa kwa simu janja Machi 19, 2025, ikionyesha moshi na moto vikifuka kwenda juu kutoka eneo la makazi kufuatia shambulizi la anga mjini Sana’a, Yemen. (Str/Xinhua)

Picha iliyopigwa kwa simu janja Machi 19, 2025, ikionyesha moshi na moto vikifuka kwenda juu kutoka eneo la makazi kufuatia shambulizi la anga mjini Sana'a, Yemen. (Str/Xinhua)

WASHINGTON - Jeffrey Goldberg, mhariri mkuu wa Jarida la The Atlantic, jana Jumatano ametoa jumbe kamili za mazungumzo ya kundi ya viongozi waandamizi wa Marekani kuhusu mpango wa operesheni ya kushambulia vikosi vya wanamgambo Wahouthi nchini Yemen, baada ya Rais Donald Trump na maafisa kadhaa wa ngazi za juu kudai mazungumzo hayo ya kundi kwenye mtandao wa Signal hayakuwa na habari za siri.

Kwenye makala yenye kichwa cha "Utawala wa Trump Kwa Bahati Mbaya Umenitumia Mipango Yake ya Vita" iliyochapishwa Jumatatu, Goldberg ameelezea namna maafisa waandamizi wa usalama wa taifa wa Marekani hivi karibuni walivyomuingiza kwenye mazungumzo ya kundi kwenye mtandao huo wa kijamii wa Signal ambalo lilikuwa likijadili shambulizi la kijeshi dhidi ya vikosi vya wanamgambo wa Wahouthi nchini Yemen. Mtandao huo wa Signal ni huduma za mawasiliano ya habari kwa siri.

Goldberg amesema kuwa Machi 15, akaunti iliyokuwa na jina la "Pete Hegseth," linalolingana na jina la waziri wa ulinzi wa Marekani, ilituma ujumbe katika mazungumzo ya kundi hilo ukiwa na maelezo kuhusu operesheni ya mashambulizi yajayo dhidi ya Yemen, yaliyokuwa yamepangwa kufanyika baada ya saa mbili. Ujumbe huo ulijumuisha habari kuhusu "maeneo lengwa, silaha ambazo Marekani itakuwa (ilikuwa imepanga) ikitumia, na utaratibu wa mashambulizi."

Goldberg hakutoa maelezo halisi ya ujumbe huo wakati huo, akisema kwamba "habari zilizomo ndani yake, kama zingesomwa na adui wa Marekani, zingeweza kutumiwa kudhuru wanajeshi na wafanyakazi wa kiintelijensia wa Marekani."

Picha iliyopigwa kwa simu janja Machi 19, 2025, ikionyesha moshi ukifuka kwenda juu kutoka eneo la makazi kufuatia shambulizi la anga mjini Sana’a, Yemen. (Str/Xinhua)

Picha iliyopigwa kwa simu janja Machi 19, 2025, ikionyesha moshi ukifuka kwenda juu kutoka eneo la makazi kufuatia shambulizi la anga mjini Sana'a, Yemen. (Str/Xinhua)

"Wataalamu wamekuwa wakituambia mara kwa mara kwamba matumizi ya mazungumzo hayo ya kundi kwenye mtandao wa Signal kwa mijadala nyeti kama hiyo yanaleta tishio kwa usalama wa taifa," Goldberg na mwenzake wamesema.

"Kama habari hizo - hasa nyakati sahihi ambazo ndege za Marekani zilikuwa zikipaa kuelekea Yemen -- zingeangukia katika mikono isiyo sahihi katika kipindi hicho muhimu cha saa mbili, marubani wa Marekani na wafanyakazi wengine wa Marekani wangeweza kuwekwa wazi kwenye hatari kubwa zaidi kuliko ambayo wangekutana nayo kawaida," wamesema.

Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Machi 5, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Machi 5, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Muda mfupi baada ya makala hiyo kuchapishwa Jumatano, Makamu Rais wa Marekani, JD Vance alijibu kwenye mitandao ya kijamii, akisema kuwa "Ni wazi kabisa Goldberg ameuza kuliko alichokuwa nacho."

Vance pia amesema kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) John Ratcliffe ameshambuliwa na Goldberg kwa kutaja jina la afisa wa CIA kwenye mazungumzo ya kundi hilo, lakini ikaja kufahamika kwamba Ratcliffe alikuwa amemtaja pekee mkuu wa ofisi yake.

Kwenye mkutano wa kutoa ushahidi na kujitetea kwa Kamati ya ujasusi ya Bunge la Seneti siku ya Jumanne, Ratcliffe alisema kwamba afisa huyo hakuwa wa siri na kwamba kuweka wazi jina lake katika mazungumzo hayo ya mtandao wa Signal ilikuwa "inafaa kabisa."

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari siku hiyo ya Jumatano, msemaji wa Ikulu ya White House ameendelea kuwa na msimamo na taarifa kwamba hakuna habari za siri katika mazungumzo hayo ya kundi. "Ujumbe huu, hakukuwa na habari za siri zilizosambazwa. Hakukuwa na mipango ya vita iliyojadiliwa," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha