

Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China akutana na viongozi wa kigeni wanaohudhuria Baraza la Boao
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akikutana na Waziri Mkuu wa Laos Sonexay Siphandone, ambaye anahudhuria mkutano wa mwaka wa Baraza la Boao la Asia 2025 unaoendelea, mjini Boao, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
BOAO, Hainan – Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amekutana jana Jumatano na viongozi wa kigeni waliofanya ziara nchini China kuhudhuria mkutano wa mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao unaoendelea huko Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China.
Ding, amefanya mkutano na Waziri Mkuu wa Laos Sonexay Siphandone. Amesema China inapenda kushirikiana na Laos katika kuunga mkono maslahi ya msingi ya kila mmoja na kuendeleza ushirikiano wa kivitendo katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake, Sonexay amethibitisha tena kwamba Laos itafanya juhudi za kila mara kupiga hatua mpya katika kuendeleza jumuiya kati ya Laos na China yenye mustakabali wa pamoja.
Kwenye mkutano na Aren B. Palik, makamu rais wa nchi ya Shirikisho la Majimbo ya Micronesia (FSM), Ding ametoa wito wa kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika biashara, uwekezaji, miundombinu na uchumi wa baharini, pia kushughulikia changamoto za Tabianchi kwa pamoja.
Palik amesisitiza kuwa nchi yake itashikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuunga mkono kithabiti misimamo ya China kuhusu suala la Taiwan na vile vile masuala yanayohusu Hong Kong, Xinjiang na Bahari ya Kusini ya China.
Kuhusu uhusiano wa China na Mongolia, Ding amemwambia Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Mongolia ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Kiuchumi Luvsannyam Gantumu kwamba uhusiano wa kudumu wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili unaendana na maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizo mbili.
Gantumu ameelezea nia ya nchi yake kuzidisha ushirikiano na China katika mawasiliano, rasilimali za nishati na sekta za teknolojia ya hali ya juu.
Kwenye mkutano na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Kazakhstan Roman Sklyar, Ding ametoa wito wa kufanya juhudi kwa pamoja kubadilisha matokeo ya Mkutano wa 12 wa hivi karibuni wa Kamati ya Ushirikiano ya China na Kazakhstan kuwa vitendo halisi.
Sklyar amesema Kazakhstan inapenda kushirikiana kwa karibu na China ili kuinua uhusiano wa pande mbili kwenye kiwango kipya.
Ding pia alikutana na Waziri Mratibu wa Indonesia wa Masuala ya Miundombinu ya Kikanda na Maendeleo, Agus Harimurti Yudhoyono na Waziri wa Nchi na Mambo ya Nje wa Ureno Paulo Rangel.
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akikutana na Waziri Mkuu wa Laos Sonexay Siphandone, ambaye yuko China kuhudhuria mkutano wa mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao unaoendelea huko Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akikutana na Aren B. Palik, Makamu Rais wa nchi ya Shirikisho la Majimbo ya Micronesia, ambaye yuko China kuhudhuria mkutano wa mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao unaoendelea huko Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akikutana na Aren B. Palik, Makamu Rais wa nchi ya Shirikisho la Majimbo ya Micronesia, ambaye yuko China kuhudhuria mkutano wa mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao unaoendelea huko Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Mongolia ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Kiuchumi, Luvsannyam Gantumur, ambaye yuko China kuhudhuria mkutano wa mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao unaoendelea huko Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Mongolia mbaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Kiuchumi, Luvsannyam Gantumur, ambaye yuko China kuhudhuria mkutano wa mwaka 2025wa Baraza la Asia la Boao unaoendelea huko Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexianga kikutana na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Kazakhstan, Roman Sklyar, ambaye yuko China kuhudhuria mkutano wa mwaka 2025 wa Baraza la Asia la Boao unaoendelea huko Boao, Mkoani Hainan, kusini mwa China, Machi 26, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma