Teknolojia za kisasa zasaidia kilimo cha majira ya mchipuko nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2025

Katika kipindi hiki wakulima katika sehemu karibu zote za China wana pilika pilika za kazi za kilimo cha majira ya mchipuko. Teknolojia za kisasa, kama vile AI, 5G, zinazojiendesha zenyewe bila ya binadamu na nyinginezo zinaonesha umahiri wao katika kazi hizo za kilimo.

Skrini ya kisasa kwenye Kituo cha Uendeshaji wa Kilimo cha Kidijitali cha Ushirika wa Kilimo wa Datian katika Wilaya ya Nanchang, Mkoa wa Jiangxi, China. (Picha na Tu Shixuan/People’s Dailly Online)

Skrini ya kisasa kwenye Kituo cha Uendeshaji wa Kilimo cha Kidijitali cha Ushirika wa Kilimo wa Datian katika Wilaya ya Nanchang, Mkoa wa Jiangxi, China. (Picha na Tu Shixuan/People's Dailly Online)

Katika Kituo cha Uendeshaji wa Kilimo cha Kidijitali cha Datian katika Wilaya ya Nanchang, Mkoa wa Jiangxi, China, roboti "Xiao Tian" kwa haraka inaonyesha taswira ya shamba kwenye skrini kubwa ya kisasa ya kituo hicho baada ya kupokea amri, na kutoa mpango unaofuata wa kazi kwa kutegemea data inayokusanywa na vihisi vilivyopo shambani.

Katika Kijiji cha Tianxing, Mkoa wa Sichuan, China kuna roboti za mbwa "Xiao Pang" na "Xiao Shou,". Ni roboti za kisasa za AI za ukaguzi kwenye mashamba ya mpunga ya kijiji hicho. Zinaweza kiotomatiki kuepuka vizuizi, kutembea kati ya matuta ya mashamba, kuchunguza kwa wakati halisi ukuaji wa mazao, kuchambua magonjwa na wadudu waharibifu, na kukusanya data ya hali ya hewa.

Roboti za kisasa za ukaguzi "Xiao Pang" (kushoto) na "Xiao Shou," (kulia) zikiwa kwenye Kijiji cha Tianxing mjini Chengdu, Mkoa wa Sichuan, China. (Picha na Wang Yuping/People’s Dailly Online)

Roboti za kisasa za ukaguzi "Xiao Pang" (kushoto) na "Xiao Shou," (kulia) zikiwa kwenye Kijiji cha Tianxing mjini Chengdu, Mkoa wa Sichuan, China. (Picha na Wang Yuping/People’s Dailly Online)

Teknolojia hizo za kisasa si tu zinafanya uzalishaji wa kilimo kuwa rahisi na sahihi zaidi, bali pia hufungua njia mpya kwa maendeleo endelevu ya kilimo.

Droni zikiweka mbolea kwa usahihi kwenye shamba la rapa katika Wilaya ya Wangjiang, Mkoa wa Anhui, China. (Picha na Chen Ruotian/People’s Dailly Online)

Droni zikiweka mbolea kwa usahihi kwenye shamba la rapa katika Wilaya ya Wangjiang, Mkoa wa Anhui, China. (Picha na Chen Ruotian/People’s Dailly Online)

Kifaa cha umwagiliaji kiotomatiki kwenye Kituo cha Upandaji na Ukuzaji wa Mboga za Majani cha Nanmudu mjini Guiyang, Mkoa wa Guizhou, China. (Picha na Tu Min/People’s Dailly Online)

Kifaa cha umwagiliaji kiotomatiki kwenye Kituo cha Upandaji na Ukuzaji wa Mboga za Majani cha Nanmudu mjini Guiyang, Mkoa wa Guizhou, China. (Picha na Tu Min/People’s Dailly Online)

Kifaa cha AI cha Kufuatilia Wadudu kikiwa kimemama kwenye Kituo cha Uzalishaji wa Miche cha Kijiji cha Gangbian mjini Zhangzhou, Mkoa wa Fujian, China. (Picha na Li Changqian/People’s Dailly Online)

Kifaa cha AI cha Kufuatilia Wadudu kikiwa kimemama kwenye Kituo cha Uzalishaji wa Miche cha Kijiji cha Gangbian mjini Zhangzhou, Mkoa wa Fujian, China. (Picha na Li Changqian/People’s Dailly Online)

Trekta inayoendeshwa na droni na droni zikifanya kazi za kilimo shambani kwenye kijiji cha Tonggui mjini Yinchuan, Ningxia, China. (Picha na Liang Hongxin/People’s Dailly Online)

Trekta inayoendeshwa na droni na droni zikifanya kazi za kilimo shambani kwenye kijiji cha Tonggui mjini Yinchuan, Ningxia, China. (Picha na Liang Hongxin/People’s Dailly Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha