China kuharakisha ujenzi wa vituo vya matumizi ya kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2025

Wateja wakichagua maboksi yenye vitu visivyoonekana kwenye duka la Pop Mart lililopo jengo kubwa la maduka mengi la Joy City katika Mtaa wa Xidan mjini Beijing, Desemba 28, 2024. (Xinhua/Shi Yifei)

Wateja wakichagua maboksi yenye vitu visivyoonekana kwenye duka la Pop Mart lililopo jengo kubwa la maduka mengi la Joy City katika Mtaa wa Xidan mjini Beijing, Desemba 28, 2024. (Xinhua/Shi Yifei)

BEIJING - Baraza la Serikali la China limetoa waraka jana Jumatano ulioandaliwa na Wizara ya Biashara ya China ili kuharakisha ugeuzaji wa kuifanya baadhi ya miji kuwa vituo vya matumizi ya kimataifa. 

Waraka huo unaeleza kuwa China itaharakisha ugeuzaji wa kuifanya miji ya Shanghai, Beijing, Guangzhou, Tianjin na Chongqing kuwa vituo vya matumizi ya kimataifa. Pia inalenga kujenga mazingira ya matumizi kwenye manunuzi yenye nguvu ya kuvutia duniani, kupanua mahitaji ya ndani na kuhimiza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu.

Unaeleza kuwa China itafanya juhudi za kuhimiza uchumi wa mambo mapya yenye kuonekana kwa mara ya kwanza. Kwa mfano, China itafanya juhudi zaidi za kuvutia chapa za ubora wa juu duniani kufungua maduka vinara nchini China, kuweka vituo vya utafiti na usanifu vya R&D na kuanzisha makao makuu ya kikanda, hivyo kuboresha mfumo wa uchumi wa mambo mapya yenye kuonekana kwa mara ya kwanza.

Waraka huo unasema, China itapanua kwa utaratibu sera ya upande mmoja wa kutoa msamaha wa visa, kuboresha mazingira yake ya matumizi kwenye manunuzi, na kuyawezesha maduka yasiyotoza kodi na sera ya kitaifa ya kurejesha malipo ya kodi ya abiria vioneshe kazi yao muhimu.

Pia inapanga kuandaa shughuli kubwa mbalimbali za kuhimiza matumizi, kuunga mkono kuandaa mashindano ya kiwango cha juu ya michezo ya kimataifa na maonyesho ya michezo ya sanaa, na kuongeza utoaji wa bidhaa na kutoa huduma bora zaidi.

Aidha, waraka huo unaeleza, China itaimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na mawasiliano ya kitamaduni. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha