Maziwa Makubwa ya Maji Baridi ya China na Afrika “mkono kwa mkono”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2025

Ziwa Poyang na Ziwa Viktoria ni maziwa makubwa zaidi ya maji baridi nchini China na barani Afrika mtawalia. Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Jiangxi, China, ambako linapatikana Ziwa Poyang, umekuwa ukiendelea kushirikiana na maeneo ya kando ya Ziwa Viktoria kueneza uzoefu wa usimamizi na maendeleo ya Ziwa Poyang.

Picha iliyopigwa Februari 13 ikionyesha mwonekano wa Ziwa Victoria jijini Mwanza, Tanzania. (Picha na Hua Hongli/Xinhua)

Picha iliyopigwa Februari 13 ikionyesha mwonekano wa Ziwa Victoria jijini Mwanza, Tanzania. (Picha na Hua Hongli/Xinhua)

Kuvuka milima na bahari, “Mkono kwa Mkono”

Xu Weimin, Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika Taasisi ya Utafiti wa Ustaarabu wa Kiikolojia ya Mkoa wa Jiangxi, ambaye alitembelea eneo la Ziwa Victoria mwaka jana, amesema kuwa hali ya sasa ya Ziwa Victoria ni kama Ziwa Poyang la zamani, likikabiliwa na changamoto kama vile mmomonyoko wa udongo na uharibifu wa ardhi oevu.

Ziwa Victoria ni moja ya vyanzo vya Mto Nile, na Ziwa Poyang ni ziwa muhimu lililounganishwa na Mto Yangtze. Maziwa hayo mawili si tu yanalisha makumi ya mamilioni ya watu katika maeneo yanayoyazunguka, bali pia yanatoa makazi kwa spishi nyingi za wanyamapori.

Katika miaka ya hivi karibuni, kwa uungaji mkono wa Kituo cha Maendeleo cha Kusini-Kusini Duniani na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Pérez-Guerrero (PGTF), Ziwa Poyang na Ziwa Victoria, yameshirikiana “mkono kwa mkono” kwa kuvuka milima na bahari.

Wataalamu kutoka mkoa huo wa Jiangxi wanachangia uzoefu na mbinu zao za Ziwa Poyang katika kushughulikia kuporomoka kwa mazingira ya kiikolojia na kuondokana na umaskini na watu wa nchi husika zinazozunguka Ziwa Victoria.

Uzoefu huu unajumuisha kualika watu kutoka nchi tatu zinazozunguka Ziwa Victoria—Uganda, Tanzania, na Kenya—kwenda katika Mkoa wa Jiangxi kujifunza kilimo cha mboga za majani zilizoongezwa thamani kubwa kama vile nyanya, pilipili, na matango; kueneza mbinu ya uzalianaji kiikolojia wa "bata kwenye shamba la mpunga" ili kudhibiti wadudu na magugu, kupunguza uchafuzi wa viuatilifu na kusaidia wakulima kuongeza kipato chao.

Ujumbe wa Ukaguzi wa Mradi wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini wa Ziwa Viktoria kutoka Idara ya Maendeleo na Mageuzi ya Mkoa wa Jiangxi, China ukikagua hali ya upandaji wa mboga za majani za oganiki katika jumuiya ya makazi mjini Kisumu, Kenya Agosti 27, 2024. (Picha kwa hisani ya Taasisi ya Utafiti wa Ustaarabu wa Kiikolojia ya Mkoa wa Jiangxi/Xinhua)

Mtafiti Mao Yuting wa Taasisi ya Utafiti wa Ustaarabu wa Kiikolojia ya Mkoa wa Jiangxi (wa pili kulia, nyuma) akieleza uzoefu wa maendeleo endelevu ya Bonde la Ziwa Poyang mjini Kisumu, Kenya Agosti 27, 2024. (Picha kwa hisani ya Taasisi ya Utafiti wa Ustaarabu wa Kiikolojia ya Mkoa wa Jiangxi/Xinhua).

Kuchangia uzoefu, kubadilika kulingana na mazingira halisi

Mjini Homa Bay, Kenya kandokando ya Ziwa Victoria, jaribio la kilimo endelevu linafanyika. Eric Ochieng, kiongozi wa "Ushirika wa Vijana wa Ukingo wa Ziwa," pamoja na wanachama wengine zaidi ya 30, wanajihusisha na ulimaji kioganiki wa mboga za majani, miwa, na maharagwe kwa usaidizi wa wataalamu wa kilimo kutoka China.

"Kutotumia mbolea za kemikali kunaweza kupunguza uchafuzi wa virutubishi vya maji ya ziwa, upandaji chini ya miti unaweza kupunguza mmomonyoko wa udongo, na mazao ya kilimo yanayokuzwa yanaweza kuuzwa kwa bei nzuri zaidi," amesema Ochieng, akiongeza kuwa, amejawa imani katika kilimo cha kioganiki kwa sababu "mbinu hizi zimethibitishwa katika Ziwa Poyang na ni zenye ufanisi mkubwa."

Ingawa kuna uwepo wa mifanano mingi, iwapo mbinu hizo za Bonde la Ziwa Poyang zinaweza kubadili ili kuendana na mazingira halisi ya kienyeji baada ya kuvuka bahari hadi maeneo ya Ziwa Victoria ni swali ambalo wataalamu wa China mara kwa mara hujiuliza.

Kwa kujikita katika mazingira na mahitaji halisi ya eneo la Ziwa Victoria, Mkoa huo wa Jiangxi ulianza kwa kutoa msaada wa kifedha na uungaji mkono wa kiufundi kwa jamii za vijijini katika eneo la Ziwa Viktoria, ili kufanya miradi midogo ya teknolojia kama vile ukarabati wa vyoo na majiko ya stovu, uhifadhi wa maji ya mvua, upandaji miti, na uzalianaji mifugo; Na hatua kwa hatua, wamesonga mbele katika uenezaji wa mbinu na dhana kama vile kilimo cha mzunguko, nishati safi, na uthibitishaji kioganiki.

Anne Okelo, afisa mradi anayehusika na maendeleo ya jamii katika shirika la Kenya la "Marafiki wa Ziwa Victoria," amesema kuwa wataalamu wa China wametoa mafunzo yenye msisitizo wa vitendo na yanayozingatia jamii, jambo ambalo limefanya mbinu ya ulinzi na uhifadhi wa Ziwa Poyang kupata matokeo makubwa katika eneo la Ziwa Victoria.

Anne Okelo, ofisa anayehusika na mradi wa maendeleo ya jamii katika Osienala (Friends of Lake Victoria) akihojiwa na shirika la habari la China, Xinhua mjini Kisumu, Kenya, Februari 19. (Picha na Li Yahui/Xinhua)

Picha iliyopigwa Februari 18 ikionenesha mandhari ya Ziwa Viktoria wakati wa machweo mjini Kisumu, Kenya. (Picha na Li Yahui/Xinhua)

Picha iliyopigwa Februari 18 ikionenesha mandhari ya Ziwa Viktoria wakati wa machweo mjini Kisumu, Kenya. (Picha na Li Yahui/Xinhua)

Mtafiti Mao Yuting wa Taasisi ya Utafiti wa Ustaarabu wa Kiikolojia ya Mkoa wa Jiangxi (kulia, mbele) akibadilishana maoni ya  hali ya utekelezaji wa mradi pamoja na Godfrey Ogonda (kushoto, nyuma), mkurugenzi wa Osienala mjini Kisumu, Kenya Desemba 19, 2019. (Picha kwa hisani ya Taasisi ya Utafiti wa Ustaarabu wa Kiikolojia ya Mkoa wa Jiangxi/Xinhua)

(Habari hii imetafsiriwa kutoka makala ya lugha ya Kichina iliyochapishwa awali na Shirika Habari la China, Xinhua, baadhi ya majina ya watu yanatafsiriwa kwa namna yanavyotamkwa.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha