

Lugha Nyingine
Rekodi ya kwanza ya chanjo ya kidijitali nchini China kwa raia wa kigeni yatolewa
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikimwonyesha mhudumu wa kujitolea (kulia) akimsaidia mfanyabiashara wa Yemen Sufyan Marwan Sufyan Mohanmmed kuchukua risiti ya kuweka miadi ya chanjo ya binti yake kutoka kwenye mashine kwa kuskani msimbo wa QR katika kituo cha huduma za afya ya eneo la makazi huko Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Machi 25, 2025. (Xinhua/Huang)
BEIJING - Sufyan Shomokh Marwan Sufyan, mtoto wa kike wa Yemen mwenye umri wa mwaka mmoja, amepokea rekodi ya chanjo ya kidijitali katika Mji wa Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, ikimfanya kuwa raia wa kwanza wa kigeni kufurahia huduma hiyo inayotolewa na China.
Uwezo wa kutoa rekodi ya chanjo ya kidijitali kwa raia wa kigeni unatokana na juhudi za vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa vya ngazi ya mikoa na miji.
Kwa kuyashinda magumu ya kiufundi katika kazi ya kubadilikabadilika kwa kulingana na hali halisi kati ya programu za kimataifa, huduma za lugha mbalimbali, utambuzi wa vitambulisho visivyo vya China, vilevile kupata rekodi za namna hiyo, China imepanua huduma hiyo ya rekodi za chanjo ya kidigitali ili kujumuisha si Wachina pekee.
"Kupata rekodi ya chanjo ya kidijitali ni kazi rahisi yenye ufanisi, na inaniruhusu kuiangalia kwenye simu yangu," amesema Sufyan Marwan Sufyan Mohanmmed, baba wa mtoto huyo wa kike, akiongeza kuwa huduma hiyo imefanya utaratibu wa kuweka miadi ya chanjo na udahili shuleni kuwa rahisi zaidi.
Kwa kuzingatia tofauti kati ya chanjo nchini China na nchi nyingine, China imefanya marekebisho yanayofaa kulingana na hali halisi kwenye mfumo wa rekodi ya chanjo, ili kukusanya taarifa kwa ufanisi na kuepuka matatizo katika chanjo ambayo yanaweza kutokea wakati watoto wanapoanza shule, wakiwemo wale waliokosa baadhi ya chanjo au kupokea chanjo za kujirudia, amesema Lou Xiaoming, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Mkoa wa Zhejiang.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma