China yagundua malimbikizo makubwa ya mafuta ya shale katika shamba kubwa la mafuta

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2025

Picha hii ya kumbukumbu ikionyesha  sehemu ya uchimbaji mafuta  kwenye eneo la kitaifa la  vielelezo vya mafuta ya shale la Jiyang katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. (Xinhua)

Picha hii ya kumbukumbu ikionyesha sehemu ya uchimbaji mafuta kwenye eneo la kitaifa la vielelezo vya mafuta ya shale la Jiyang katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. (Xinhua)

JINAN – Shirika la Mafuta ya Petroli na Kemikali la China (Kundi la Kampuni za Sinopec), shirika kubwa zaidi la kusafisha mafuta nchini China, limetangaza kugundua shamba la mafuta ya shale liliyothibitishwa yenye ujazo wa tani zaidi ya milioni 140 katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China.

Hili ni shamba la kwanza la mafuta ya shale lenye akiba iliyothibitishwa ambayo imezidi ujazo wa tani milioni 100 kuweza kuidhinishwa na Wizara ya Maliasili ya China, na mafanikio makubwa katika utafutaji wa mafuta na gesi katika eneo la kitaifa la vielelezo vya mafuta ya shale la Jiyang.

Hadi kufikia sasa, makadirio ya maliasili ya mafuta ya shale yamefikia ujazo wa tani bilioni 10.5 katika eneo hilo la vielelezo linalomilikiwa na Shamba la Mafuta la Shengli mkoani Shandong, huku pato la mafuta likizidi ujazo wa tani milioni moja.

"Makadirio ya akiba ya mafuta ya shale ya Shamba la Mafuta la Shengli ni sawa na maliasili za kawaida za mafuta na gesi zilizogunduliwa kwenye Shamba la Mafuta la Shengli katika zaidi ya miaka 60 iliyopita," amesema Sun Yongzhuang, mkuu msaidizi wa Sinopec na mkurugenzi mtendaji wa Idara ya Usimamizi wa Shamba la Mafuta ya Petroli la Shengli.

Shamba la Mafuta la Shengli liligunduliwa mwaka 1961, na likahuishwa kuanzia d mwaka 1964.

Mafuta ya shale hasa hurejelea hidrokaboni kimiminika ambazo zimenaswa chini ya ardhi kwenye ngazi ya miamba ya shale zinazoweza kutolewa kwa kusafishwa. Katika hali ya kawaida mafuta hayo yanapatikana katika miamba hiyo ya shale yenye wingi wa oganiki na matabaka fungani myembamba ya miamba ya kaboneti, mchanga wa mawe na mawe yenye uoevu.

China imeanzisha maeneo matatu ya ngazi ya kitaifa ya vielelezo vya mafuta ya shale katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Mkoa wa Heilongjiang na Mkoa wa Shandong, mtawalia. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha