Roboti za kugema mpira zinazowezeshwa na AI zasanifiwa kupunguza uhaba wa nguvukazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2025

Picha iliyopigwa Machi 4, 2025 ikionesha roboti jongefu ya kugema mpira wa asili mjini Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China.   Ikiwa imeundwa kwa pamoja na Akademia ya Sayansi za Kilimo cha Kitropiki ya China (CATAS) na kampuni ya teknolojia ya Automotive Walking Technology yenye makao yake mjini Beijing, roboti hiyo ya kujiendesha yenyewe iko tayari kufanyiwa majaribio kwenye mashamba ya zao la mpira mkoani Hainan wakati wa msimu wa mavuno mwezi Aprili. (Xinhua/Yang Guanyu)

Picha iliyopigwa Machi 4, 2025 ikionesha roboti jongefu ya kugema mpira wa asili mjini Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. Ikiwa imeundwa kwa pamoja na Akademia ya Sayansi za Kilimo cha Kitropiki ya China (CATAS) na kampuni ya teknolojia ya Automotive Walking Technology yenye makao yake mjini Beijing, roboti hiyo ya kujiendesha yenyewe iko tayari kufanyiwa majaribio kwenye mashamba ya mpira mkoani Hainan wakati wa msimu wa mavuno mwezi Aprili. (Xinhua/Yang Guanyu)

Ili kukabiliana na uhaba wa wafanyakazi unaoathiri tasnia yake ya zao la mpira wa asili, China imeonesha kwa umma roboti jongefu ya kugema mpira, ikiwa hatua kubwa katika teknolojia ya kiotomatiki kwenye kilimo.

Ikiwa imeundwa kwa ushirikiano kati ya Akademia ya Sayansi za Kilimo cha Kitropiki ya China (CATAS) na kampuni ya teknolojia ya Beijing Automotive Walking Technology, roboti hiyo ya kujiendesha kiotomatiki iko tayari kuanza majaribio katika mashamba ya mpira mkoani Hainan mwezi Aprili, wakati wa msimu wa uvunaji.

Katika video ya kuonesha ufanyaji wake kazi, roboti hiyo inaonekana ikielekea kwenye mti wa mpira, kabla ya kusimama kwa usahihi wa hali ya juu, na kisha kunyoosha mkono wake wa kiroboti kufanya mjongeo wa kugema kwa usahihi gome la mti. Ndani ya sekunde chache baada ya mjongeo huo wa ugemaji, utomvu mweupe wa mpira ukaanza kutiririka kutoka kwenye mti huo.

Sekta ya mpira wa asili ya China, ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa matairi na chanzo cha mahitaji mengine ya viwandani, kwa sasa inakabiliwa, na nakisi kubwa ya nguvukazi kutokana na mazingira magumu ya kazi, zamu za usiku, na kiwango kikubwa cha magonjwa ya kazi yanayoathiri wavunaji wa mpira.

"Roboti hizi zimebuniwa mahsusi kushughulikia uhaba wa wagemaji wa mpira, ambao umekuwa tatizo kubwa kwa tasnia hii," amesema Cao Jianhua, naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mpira ya CATAS.

Roboti inatumia kikamilifu teknolojia zinazoendeshwa na AI kuendana na maeneo magumu na kufanya ugemaji kwa usahihi.

Kwa mujibu wa Cao, kampuni kadhaa za kimataifa za matairi na wakulima wa mpira kutoka Asia Kusini-Mashariki, ikiwemo Indonesia na Thailand, zimeonyesha hamu kubwa ya kutumia teknolojia hiyo.

Picha iliyopigwa Machi 4, 2025 ikionesha roboti jongefu ya kugema mpira mjini Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu)

Picha iliyopigwa Machi 4, 2025 ikionesha roboti jongefu ya kugema mpira mjini Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu)

Picha iliyopigwa Machi 4, 2025 ikionesha roboti ya kuvuna mpira inayoweza kutembea huko Haikou, Mkoa wa Hainan wa Kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu)

Picha iliyopigwa Machi 4, 2025 ikionesha roboti ya kuvuna mpira inayoweza kutembea huko Haikou, Mkoa wa Hainan wa Kusini mwa China. (Xinhua/Yang Guanyu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha