Trump asema anaweza "kutoa misamaha kwa nchi nyingi" juu ya ushuru

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 25, 2025

Rais wa Marekani Donald Trump akiondoka baada ya shughuli ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Ugiriki kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Machi 24, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Rais wa Marekani Donald Trump akiondoka baada ya shughuli ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Ugiriki kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Machi 24, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

WASHINGTON - Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba anaweza "kutoa msamaha wa ushuru kwa nchi nyingi", wakati tarehe yake ya mwisho ya Aprili 2 ya kuweka "ushuru wa kutozana sawa" kwa washirika wa biashara wa Marekani ikikaribia.

"Ninaweza kutoa msamaha wa ushuru kwa nchi nyingi, lakini ushuru utatozwa kwa usawa ," Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House Jumatatu mchana.

Amebainisha kuwa Umoja wa Ulaya (EU) umekubali kupunguza ushuru wa magari hadi asilimia 2.5 kama sehemu ya makubaliano na serikali ya Marekani.

"Tutakuwa tukitangaza ushuru wa ziada katika siku chache zijazo, unaohusiana na magari, na pia mazao ya mbao njiani, mbao na chipu," Trump ameendelea kusema.

"Lakini kwa sehemu kubwa, Aprili 2 itakuwa siku kubwa, ambayo itakuwa siku ya kutozana ushuru kwa usawa, na tutakuwa tukirudisha kiasi cha pesa ambazo zimechukuliwa kutoka kwetu," Trump amesema.

Mapema siku hiyo, Trump alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba atatoza ushuru wa asilimia 25 kwa nchi zote zinazonunua mafuta na/au gesi kutoka Venezuela, akiishutumu nchi hiyo ya Amerika Kusini kwa kutuma "makumi ya maelfu ya" wahalifu nchini Marekani.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari kama ushuru huo wa asilimia 25 ni "juu ya ushuru uliopo," Trump alisema "ndiyo."

Huku viashiria muhimu vya kiuchumi vya Marekani vikionyesha mwelekeo wa wasiwasi, wachumi na wawekezaji wanaonya kwamba hatari ya "Mdororowatrump" (Trumpcession) imeongezeka kutokana na sera za kiuchumi na kibiashara zisizotabirika.

Mapema mwezi huu, Bruce Kasman, mwanauchumi mkuu wa kimataifa wa JPMorgan, alielezea wasiwasi mkubwa kuhusu uchumi wa Marekani. Aliwaambia waandishi wa habari nchini Singapore kwamba benki ya uwekezaji sasa inakadiria uwezekano wa kupungua kwa asilimia 40 ya uchumi wa Marekani mwaka huu. 

Rais wa Marekani Donald Trump akihudhuria shughuli ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Ugiriki kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Machi 24, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Rais wa Marekani Donald Trump akihudhuria shughuli ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Ugiriki kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Machi 24, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha