Kampuni ya magari ya Audi yaimarisha uzalishaji wa NEV nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 25, 2025

Picha iliyopigwa Machi 21, 2025 ikionyesha karakana ya uchomeleaji ya Kampuni ya magari ya nishati mpya NEV ya Audi FAW mjini Changchun, Mkoani Jilin, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Si Xiaoshuai)

CHANGCHUN - Kwenye karakana za kiwanda cha kwanza cha Kampuni ya Magari ya Audi mahsusi kwa ajili ya uzalishaji wa magari yanayotumia nishati ya umeme (NEVs) nchini China, kipande kizima za chuma hugeuzwa kwa haraka sana kuwa sehemu za magari kwa mashine za kusukuma, huku mikono ya roboti ikifanya kazi kwa usahihi kwenye mstari wa kuunganisha sehemu za magari, ulioandaliwa kwa ajili ya kuzalisha gari jipya la Audi Q6L e-tron.

Gari hilo la SUV linalotumia nishati ya umeme, lililosanifiwa mahsusi kwa ajili ya soko la China, limeundwa kwenye Premium Platform Electric (PPE) katika kiwanda cha Kampuni ya NEV ya Audi FAW mjini Changchun, mji mkuu wa Mkoa wa Jilin, kaskazini mashariki mwa China. Linatarajiwa kuingia sokoni baadaye mwaka huu.

Helmut Stettner, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya NEV ya Audi FAW alijiunga na FAW-Volkswagen, kampuni mama ya Audi, mjini Changchun mwaka 2011 akiwa mkurugenzi wa kiwanda na uzalishaji, akipata maarifa muhimu kuhusu hali ya kipekee ya soko la China. Muongo mmoja baadaye, mwaka 2021, alirudi kuongoza mradi wa PPE wa Audi, akisukuma mbele maendeleo ya magari yanayotumia nishati mpya.

Stettner amesema kampuni hiyo inashirikiana kikamilifu na washirika wa ndani kutengeneza bidhaa mpya, ikijitahidi kujumuisha ubunifu wa hali ya juu wa China kwa haraka. Amefafanua kuwa, kuanzia mwaka huu, miundo ya Audi iliyojengwa kwenye jukwaa hilo la PPE kwa soko la China itakuwa na mfumo wa teknolojia za hali ya juu za usaidizi wa kuendesha gari unaowezeshwa na teknolojia ya Huawei.

Kwa miaka mingi, Stettner ameshuhudia mapito ya hali mbalimbali ya ushirikiano wa magari kati ya China na Ujerumani na maendeleo ya kasi ya sekta ya magari ya China.

"Mwaka 1988, tulikuwa kampuni ya kwanza ya kigeni inayozalisha magari ya hali ya juu nchini China. Tangu wakati huo, tumekuwa tukipanua ushirikiano na uwepo wetu wa ndani na kuzindua modeli nyingi mpya na washirika wetu, siku zote umechanganya nguvu za nchi hizo mbili," Stettner ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Stettner amesema kuhama kutoka magari ya kawaida kwenda kwa magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) katika sekta ya magari ya kimataifa kumeleta fursa mpya kwa China na Ujerumani.

Stettner amesisitiza kuwa "sera ungaji mkono za serikali zimetoa mchango muhimu katika kuendeleza soko la NEV la China," zikiwemo juhudi katika miundombinu ya kuchaji, kuendesha gari kiotomatiki, na magari yaliyounganishwa na teknolojia za kisasa.

Mfanyakazi akiendesha kifaa kwenye karakana ya uchomeleaji ya Kampuni ya NEV ya Audi FAW mjini Changchun, Mkoani Jilin, kaskazini mashariki mwa China, Machi 21, 2025. (Xinhua/Si Xiaoshuai)

Mfanyakazi akiendesha kifaa kwenye karakana ya uchomeleaji ya Kampuni ya NEV ya Audi FAW mjini Changchun, Mkoani Jilin, kaskazini mashariki mwa China, Machi 21, 2025. (Xinhua/Si Xiaoshuai)

Helmut Stettner, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NEV ya Audi FAW, akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua mjini Changchun, Mkoani Jilin, kaskazini mashariki mwa China, Machi 20, 2025. (Xinhua/Si Xiaoshuai)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha