

Lugha Nyingine
Marekani yafanya shambulizi la anga dhidi ya mji mkuu wa Yemen
(CRI Online) Machi 24, 2025
Televisheni ya al-Masirah inayoendeshwa na kundi la wanamgambo Wahouthi imeripoti kuwa Marekani imefanya shambulizi la anga Jumapili usiku dhidi ya jengo la makazi lililopo kwenye mji mkuu Sana'a unaodhibitiwa na kundi hilo la wanamgambo nchini Yemen, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 15 kujeruhiwa.
Televisheni hiyo imeinukuu idara ya afya inayodhibitiwa na kundi la Houthi ikisema kuwa, takwimu za awali zinaonyesha kuwa “watoto watatu na wanawake wawili” ni miongoni mwa majeruhi wa shambulizi hilo dhidi ya eneo la Asr, magharibi mwa Sana'a.
Wakazi wenyeji wamesema shambulizi hilo ni kali sana, na timu za uokoaji bado zinatafuta manusura chini ya vifusi.
Jeshi la Marekani bado halijatoa tamko lolote.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma