

Lugha Nyingine
China Yaidhinisha Helikopta ya Kwanza Inayojiendesha bila Rubani
Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Oktoba 2022 ikionesha helikopta ya koaksia (coaxial) ya TD550 inayojiendesha bila rubani ikiwa kwenye urukaji wa majaribio juu ya nyanda za juu mjini Hetian, Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China. (Xinhua)
Mfumo wa helikopta inayojiendesha bila rubani ya TD550D ya muundo wa pande mbili za mapanga (coaxial) umepokea cheti cha ithibati cha muundo wake kutoka kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC), ukiwa ni wa kwanza wa aina yake kupata idhini hiyo nchini China, imesema kampuni ya United Aircraft, muundaji wake siku ya Ijumaa.
Tian Gangyin, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya United Aircraft, amesema kwamba idhini hiyo inajaza pengo katika uidhinishaji stahiki wa kuruka angani kwa mifumo hiyo ya helikopta zinazojiendesha bila rubani nchini China, ikiweka kiwango rejea kwa uidhinishaji wa baadaye wa helikopta kama hizo.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, TD550D inajivunia uwezo mkubwa wa kubeba mizigo, ustahimilivu wa kuendeshwa wa muda mrefu, na ufanisi mzuri kwenye eneo la juu angani, jambo linaloifanya ifae kwa mazingira yenye changamoto kama vile nyanda za juu na visiwa.
Ndege hiyo, iliyoundwa mahsusi kwa matumizi katika uokoaji wa dharura, kuzima moto, na usafirishaji wa mizigo kwa teknolojia ya kisasa, ina sifa za kurudi kwa dharura, kutua kiotomatiki, na uwezo wa kutua kwa kuamriwa katika hali hatarishi.
Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa Juni 2024 ikionesha helikopta ya koaksia (coaxial) ya TD550 inayojiendesha bila rubani ikishiriki kwenye uokoaji wa dharura mjini Huangshan, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)
Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa Oktoba 2023 ikionesha helikopta ya koaksia (coaxial) ya TD550 inayojiendesha bila rubani ikishiriki kwenye uoneshaji wa namna ya kuzimamoto mjini Huangshan, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma