

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China aahidi ufunguaji mlango zaidi wakati wa kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika duniani
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Maendeleo la China 2025 na kutoa hotuba mjini Beijing, Machi 23, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Jumapili kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa Jukwaa la Ngazi ya Juu la Maendeleo la China 2025 mjini Beijing, ameahidi kuhimiza kwa uthabiti ufunguaji mlango na ushirikiano wakati wa kuongezeka kwa hali isiyo ya utulivu na kutokukwa na uhakika duniani.
"China itaendelea kukaribisha kwa mikono miwili kampuni kutoka sehemu mbalimbali duniani, kupanua zaidi ufikiaji wa soko, kufanya juhudi za kushughulikia masuala yanayofuatiliwa na kampuni, na kuwezesha viwanda vinavyowekezwa na nje kujumuishwa kwa kina katika soko la China," amesema.
Ameeleza kuwa, kuzidishwa kwa mafarakano ya uchumi duniani, pamoja na kuongezeka kwa hali isiyo ya utulivu na kutokuwa na uhakika katika dunia ya leo, kumeonesha mahitaji yanayoongezeka kwa nchi kufungua masoko yao na kwa viwanda kunufaika pamoja na rasilimali, ili kukabiliana na changamoto na kutafuta ustawi kwa pamoja.
"China italinda biashara huria, na kuchangia katika uendeshaji mzuri na tulivu wa minyororo ya viwanda na ya utoaji bidhaa katika Dunia." amesema
China imeweka lengo lake la ongezeko la asilimia 5 hivi la mwaka mzima wa 2025 , Li amesema, akiongeza kuwa uamuzi huo unaonyesha kuwa, China imeelewa kwa kina hali yake ya kimsingi ya uchumi na kuwa na imani kubwa kwa uwezo wake wa usimamizi na uwezekano wa maendeleo ya siku za baadaye. Ameahidi kufanya juhudi za kuimarisha uungaji mkono wa sera wakati huohuo kuchochea nguvu za soko ili kufikia lengo hilo.
Li amesema, "China itatekeleza sera za jumla zenye hamasa na matokeo zaidi, kuimarisha zaidi marekebisho ya kukabiliana na mzunguko, na kuanzisha sera mpya za nyongeza wakati inapohitajika ili kutoa uungaji mkono wa kithabiti kwa uboreshaji endelevu na uendeshaji wa uchumi wa hatua madhubuti," Li amesema.
Amesisitiza kuwa, China itaendelea kuhimiza ujenzi wa soko kubwa la pamoja la kitaifa na kuondoa vizuizi katika mzunguko wa uchumi ili kujenga mazingira bora ya maendeleo kwa mashirika mbalimbali ya biashara.
Jukwaa la Ngazi ya Juu la Maendeleo la China 2025 limepangwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Tarehe 23 hadi 24 Machi. Kaulimbiu ya jukwaa hilo la mwaka huu ni "Kufungua Nguvu ya Maendeleo kwa Ongezeko Tulivu la Uchumi Duniani"
Watu karibu 720, wakiwemo wajasiriamali, maofisa wa serikali, wataalam na wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa ya ndani na nje ya China walihudhuria kwenye ufunguzi wa jukwaa hilo, lililoandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Maendeleo cha Baraza la Serikali la China.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Ngazi ya Juu la Maendeleo la China 2025 na kutoa hotuba mjini Beijing, Machi 23, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma