

Lugha Nyingine
Mkuu wa Idara ya kupambana na ufisadi ya China asisitiza kuimarisha usimamizi wa chama na mapambano dhidi ya ufisadi
Li Xi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, akitembelea Kijiji cha Wangkou cha Wilaya ya Wuyuan katika mji wa Shangrao, Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China, Machi 18, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)
NANCHANG - Li Xi, mkuu wa Katibu wa kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ametoa maagizo ya kufanya juhudi madhubuti kwa mashirika ya ukaguzi na usimamizi wa nidhamu ya nchi hiyo kufanya kampeni ya elimu ili kutekeleza "uamuzi wa mambo nane" wa kamati kuu ya chama juu ya kuboresha maadili ya kazi, kuhimiza usimamizi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa ukali, na kupambana na ufisadi.
Li ametoa wito huo katika ziara ya ukaguzi Mkoani Jiangxi, mashariki mwa China, kuanzia Jumatatu hadi jana Alhamisi.
Wakati akitembelea sehemu mbalimbali za mkoa huo, Li amehimiza mashirika ya ukaguzi na usimamizi wa nidhamu kuendelea kuzidisha udhibiti wa vitendo vya ukiukaji sheria na rushwa miongoni mwa watu, na kutekeleza majukumu yao ya uangalizi vizuri ili kuongeza kasi ya kazi ya kuboresha maadili, kuimarisha uadilifu na mapambano dhidi ya ufisadi katika mashirika yanayomilikiwa na serikali.
Kwenye kongamano lililofanyika katika ziara hiyo, Li ametoa wito kwa mashirika hayo ya ukaguzi na usimamizi wa nidhamu katika ngazi zote kuzidisha usimamizi wa kisiasa na kupata mafanikio mapya na makubwa zaidi katika utekelezaji wao wa kujisimamia kikamilifu na kwa ukali kwa CPC.
Pia ameyahimiza kuimarisha uwezo wao wa kisiasa, uelewa wao wa sera, na maarifa yao ya nidhamu na sheria.
Li Xi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, akiongoza kongamano mjini Nanchang, Mkoani Jiangxi, mashariki mwa China, Machi 20, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma