

Lugha Nyingine
Rais Xi wa China ahimiza kuanzisha hali mpya ya maendeleo ya Yunnan wakati wa ziara yake ya ukaguzi mkoani humo
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza na wakazi wenyeji wakati akitembelea eneo la Mji Mkongwe la Mji Lijiang katika Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
KUNMING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) katika ziara yake ya ukaguzi katika Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China Jumatano na Alhamisi amehimiza Mkoa huo kuanzisha hali mpya ya maendeleo yake katika mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Siku ya Jumatano mchana, Rais Xi alitembelea eneo maalum la shughuli za kisasa za kupanda na kuuza maua katika mji wa Lijiang.
Katika kituo cha maonyesho, Rais Xi alifahamishwa kuhusu aina mbalimbali za maua freshi ya kukatwa. Pia alikagua eneo la kupanda maua ya waridi na mstari wa upangaji wa ngazi tofauti na ufungashaji wa maua hayo ya waridi katika eneo hilo maalum.
"Shughuli za maua za Yunnan zina matarajio mapana,” Rais Xi amesema, akisisitiza umuhimu wa kuanzisha na kuendeleza mnyororo mzima wa shughuli za maua ili "shughuli hizo za kupendeza" ziweze kuleta manufaa zaidi kwa watu.
Ukiwa umewekwa kwenye Orodha ya UNESCO ya Mali ya Urithi wa Kitamaduni wa Dunia, Mji Mkongwe wa Lijiang umekuwa na historia ya miaka zaidi ya 800. Akitembelea mji huo mkongwe, Rais Xi alifahamishwa kuhusu historia yake na nyumba za mtindo wa kipekee za watu wa kabila la Wanaxi. Pia alifahamishwa kuhusu juhudi za wenyeji katika kuhifadhi na kutumia kikamilifu mali ya urithi wa kitamaduni, na katika kuhimiza maendeleo ya shughuli jumuishi za utamaduni na utalii.
Ikiwa ni punde tu kuanza kwa majira ya mchipuko sasa, mji huo ulikuwa umejaa watalii. Rais Xi alizungumza na wakazi wenyeji na watalii katika mji huo, akiuliza kuhusu hali ya biashara za wenyeji na maoni ya watalii katika matembezi yao.
Amesisitiza kushughulikia vizuri uhusiano kati ya ulinzi na maendeleo ili kuufanya mji huo mkongwe wenye kupendeza ung'ae kwa nguvu na uhai mpya.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi, Rais Xi pia alitembelea mji mkuu wa mkoa huo, Kunming, ambako alisikiliza ripoti ya kazi za kamati ya chama ya mkoa Yunnan na serikali ya mkoa huo siku ya Alhamisi.
Amesisitiza kwamba kuhimiza mageuzi na uboreshaji wa viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya sifa bora , akitoa wito kwa Yunnan kuimarisha, kuboresha na kupanua viwanda vyake vinavyotegemea rasilimali zake kupitia uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, wakati huohuo ikiendeleza kwa bidii viwanda vya siku za baadaye na vile vinavyoibukia vya kimkakati.
Ameuhimiza mkoa huo kuharakisha maendeleo ya shughuli jumuishi za utamaduni na utalii, na kazi za kilimo zenye umaalumu wa eneo la uwanda wa juu.
Jana Alhamisi, Rais Xi alikutana na maofisa waandamizi na wajumbe wa wanajeshi na wafanyakazi wa kiraia wa vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China vilivyoko Kunming.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza na wakazi wenyeji na watalii wakati akitembelea eneo la Mji Mkongwe la Mji Lijiang, katika Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitembelea eneo maalum la shughuli za kisasa za maua katika Mji Lijiang, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza na wakazi wenyeji na watalii wakati akitembelea eneo la Mji Mkongwe la Mji Lijiang, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akifahamishwa kuhusu utamaduni wa watu wa kabila la Wanaxi kwenye maonyesho wakati akitembelea eneo la Mji Mkongwe la Mji Lijiang Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiuliza kuhusu hali ya biashara za wenyeji wakati akitembelea eneo la Mji Mkongwe la Mji Lijiang Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza na wakazi wenyeji na watalii wakati akitembelea eneo la Mji Mkongwe la Mji Lijiang Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Machi 19, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma