

Lugha Nyingine
Uzuri wa Majira: Kipindi cha Chunfen
Habari, kila mmoja! Mimi ni Sisi, mpenda kusafiri! Leo ni Chunfen, au siku mlingano wa usiku na mchana ya majira ya mchipuko, kipindi cha nne katika vipindi vya hali ya hewa kwa kalenda ya kilimo ya China na siku ya uwiano kati ya mwanga na joto. Ungana nami tukitembelea Mji wa Wuhan, Mkoa wa Hubei wa katikati mwa China, na kuona uzuri wake wa kipekee katika majira ya Mchipuko!
Mwezi Machi, maua ya cheri huwa katika mchanuo kamili mjini Wuhan. Kwenye Bustani ya Maua ya Cheri ya Ziwa Mashariki, maua hayo hufunika njia, hupeperuka kuvuka pande za milima, na huakisiwa kwenye maji ya ziwani, yakipaka bustani nzima rangi za mchipuko. Upepo hubeba harufu nzuri ya maua hayo, ikiufunika mji kwa mguso laini wa msimu.
Kipindi cha Chunfen ni wakati wa matembezi ya nje na kurusha tiara. Kwenye Njia ya Kijani ya Ziwa Mashariki, tiara zenye rangi hupepea angani; kando ya Daraja la Mto Yangtze, wakimbiaji hufurahia hamasa ya mchipuko. Jiji zima huamka kwa uhai.
Watu wa kale walikichukulia kipindi cha Chunfen kama wakati wa msawazisho, ambao ni muda mwafaka wa kutengeneza pombe. Asubuhi na mapema katika Mtaa wa Hubu, hewa hujaa harufu nzuri ya mvinyo wa mchele na maua mabichi ya sophora. Bakuli moja la mvinyo wa mchele, mtafuno mmoja wa tambi kavu za moto za Wuhan zilizo na siagi ya ufuta — hata kifungua kinywa kinabeba utamu wa mchipuko.
Siku hiyo pia husherehekewa na dunia. Kwa mfano, Nowruz, hugongana wakati mmoja sawa na Chenfun, ni Mwaka Mpya wa Asia ya Kati kuukaribisha msimu wa mchipuko. Katika siku hii, nchi nyingi kama Iran, India, Tajikistan, na Afghanistan husherehekea ukuaji wa kila kitu na matumaini kwa mustakabali mzuri.
Kutoka kwenye Mnara wa Korongo wa Njano, ninatazama maji ya Yangtze yaliyopashwa joto la msimu wa mchipuko na anga isiyo na mwisho. Kwenu mliombali, nitakamata mambo bora ya mchipuko hapa na kuyafunga ndani ya ujumbe huu: "Kama mgeni wa heshima, upepo wa majira ya mchipuko hutuletea ustawi mara unapowasili."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma