

Lugha Nyingine
Mkutano wa uhimizaji wa hamasa mjini Milan, Italia waangazia Maonyesho ya China ya Minyororo ya Utoaji wa Bidhaa ya Kimataifa
Mario Boselli, mwenyekiti wa Taasisi ya Baraza la China na Italia, akizungumza kwenye mkutano wa uhimizaji wa hamasa wa Maonyesho ya tatu ya China ya Minyororo ya Utoaji wa Bidhaa ya Kimataifa (CISCE) mjini Milan, Italia, Machi 18, 2025. (Xinhua/Li Jing)
MILAN, Italia – Mkutano wa uhimizaji wa hamasa wa Maonyesho ya tatu ya China ya Minyororo ya Utoaji wa Bidhaa ya Kimataifa (CISCE) umefanyika Jumanne mjini Milan, Italia, huku ushirikiano wa pande mbili ukiangaziwa na makubaliano kadhaa ya ushirikiano yamesainiwa.
Wawakilishi zaidi ya 200 kutoka taasisi za kukuza biashara na uwekezaji, mashirikisho ya wafanyabiashara na kampuni za China na Italia walishiriki kwenye mkutano huo.
Ren Hongbin, mwenyekiti wa Kamati ya Uhimizaji wa Biashara ya Kimataifa ya China amedhihirisha kuwa, maendeleo ya hatua madhubuti yamepatikana katika ushirikiano wa pande mbili tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Italia miaka 55 iliyopita.
Ren Hongbin, mwenyekiti wa Kamati ya Uhimizaji wa Biashara ya Kimataifa ya China, akizungumza kwenye mkutano wa uhimizaji wa hamasa wa Maonyesho ya tatu ya China ya minyororo ya utoaji wa bidhaa ya Kimataifa huko Milan, Italia, Machi 18, 2025. (Xinhua/Li Jing)
Ren pia amehimiza ushirikiano zaidi katika sekta za jadi wakati huohuo kupanua ushirikiano katika nyanja zinazoibuka kama vile magari yanayotumia nishati ya umeme, teknolojia ya AI, na uchumi wa kidigitali.
Wawakilishi wa Italia wamesisitiza uhusiano imara wa pande mbili kati ya Italia na China. Wakati changamoto za siasa za kijiografia zinazidiwa siku hadi siku na hali ya uchumi wa Dunia kutokuwa na uhakika, wanatarajia majukwaa kama CISCE kusaidia kujenga ushirikiano wa karibu kwenye minyororoo ya utoaji wa bidhaa ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Italia na China na Ulaya.
Watu wakihudhuria mkutano wa uhimizaji wa hamasa wa Maonyesho ya tatu ya China ya minyororo ya utoaji bidhaa ya Kimataifa mjini Milan, Italia, Machi 18, 2025. (Xinhua/Li Jing)
Maonyesho ya tatu ya China ya minyororo ya utoaji wa bidhaa ya Kimataifa yaliyopangwa kufanyika Julai 16-20 mwaka huu mjini Beijing, yanatarajiwa kuweka mkazo katika kufuatilia minyororo ya utoaji wa bidhaa za viwanda vya teknolojia ya hali ya juu, nishati safi, magari ya teknolojia ya AI , teknolojia ya kidigitali, maisha ya afya na kilimo cha kijani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma