Kifaa kinachosaidia kutembea kama "Cyborg" chalenga soko linalopanuka la wazee la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 19, 2025

Mzee aliyevalia kifaa kinachomsaidia kutembea akifanya manunuzi kwenye soko mjini Hangzhou, Mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, Februari 24, 2025. (RoboCT/kupitia Xinhua)

Mzee aliyevalia kifaa kinachomsaidia kutembea akifanya manunuzi kwenye soko mjini Hangzhou, Mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, Februari 24, 2025. (RoboCT/kupitia Xinhua)

HANGZHOU –"Cyborg" katika hadithi za kisayansi, ambazo hapo awali zilikuwa alama za uwezo wa hali ya juu wa kibinadamu, sasa zinawezesha mapinduzi ya utunzaji wazee ya China huku uchumi wa nchi hiyo unaohusu mambo ya wazee ukistawi.

Kifaa kinachosaidia kutembea cha exoskeleton kilichoundwa na kampuni mpya ya ubunifu ya RoboCT inayopatikana mjini Hangzhou, Mkoani Zhejiang mashariki mwa China, kinaweza kufanya utalii wa kupanda milima kuwa rahisi kwa wazee kwa kukabiliana na uzito wa chupa tano za maji kwa kila kuinua mguu.

RoboCT inapanga kuzindua uvumbuzi wake huo mpya mwishoni mwa mwezi huu. Kinauzwa kwa bei nafuu ya yuan 2,000 (dola takriban 276 za Kimarekani). Katika mji huo ambao ni kituo kikuu cha teknolojia mashariki mwa China, kampuni zaidi kama RoboCT zinatengeneza roboti zinazolenga kusaidia matembezi ya wazee.

Wahandisi wa RoboCT waligundua kuwa wazee wengi wanatembea kwa migongo iliyopinda, kupiga hatua ndogo na kutumia vishikizi vya kiuno kwenye nyumba za kutunza wazee, na kwa hivyo walielekeza juhudi za usaidizi wa kifaa hicho kwenye kiuno, mgongo na nyonga.

"Bidhaa hiyo inasaidia ukunjaji wa nyonga na kutuliza uti wa mgongo ili kusaidia wazee kutembea kwa kasi, hatua za haraka na utulivu mkubwa," amesema Yan Hai, mkurugenzi wa bidhaa wa RoboCT, katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua.

Kikitengenezwa kwa kuigilizia mwenendo wa kano za mwili, kifaa hicho kisichotumia betri, chenye uzito wa kilo 2, kinavaliwa kuzunguka nyonga na juu ya magoti, kikinasa na kuhifadhi baadhi ya nishati inayotokana na mwili, kabla ya kuitoa ili kusaidia kutembea.

Idadi ya wazee ya China inayozidi kuongezeka inakabiliwa na ongezeko la mahitaji yanayopanuka ya kutembea ambayo hayajafikiwa, ikisababisha kulemewa mzigo kwa wahudumu wa tiba mwili na upungufu wa wahitimu wa tiba hiyo kila mwaka.

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka 2024, idadi ya watu wa China wenye umri wa miaka 60 na zaidi ilikuwa imefikia milioni 310 – ikichukua karibu asilimia 22 ya jumla ya watu wake.

Kampuni zinazozidi kuongezeka za China zimeona fursa kubwa za biashara zinazotokana na ongezeko la watu wanaozeeka. Uchumi wa nchi hiyo unaotegemea wazee na kuendelea unaibuka kuwa kichocheo kikuu cha ukuaji, na kwa sasa thamani yake imefikia yuan trilioni 7.

Kwa mujibu wa utafiti kutoka shirika la kutoa huduma za uchambuzi wa data iiMedia Research, uchumi wa China unaohusu mambo ya wazee wa umri huo unatarajiwa kufikia kiwango cha yuan trilioni 30 ifikapo mwaka 2035.

Mzee aliyevalia kifaa kinachosaidia kutembea akipanda ngazi mjini Hangzhou, Mkoani Zhejiang, mashariki mwa China, Februari 24, 2025. (RoboCT/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha