

Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini ataka ripoti kamili kutoka kwa Balozi wa nchi hiyo aliyefukuzwa kutoka Marekani
(CRI Online) Machi 18, 2025
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa Balozi wa nchi hiyo nchini Marekani Ebrahim Rasool ambaye amefukuzwa nchini humo atampa maelezo kamili kuhusu hali halisi ya sasa.
Akizungumza katika mkutano wa kilele wa Maendeleo ya Uongozi kwa Watoto wa Bana Pele mjini Johannesburg, Rais Ramaphosa amerejelea tena ahadi ya nchi yake ya kushirikiana na serikali ya Marekani, akielezea kufukuzwa kwa Balozi Rasool kama kikwazo kidogo katika uhusiano wa pande mbili hizo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma