Rwanda yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ubelgiji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2025

Rwanda imevunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ubelgiji na kuamuru wanadiplomasia wote wa Ubelgiji kuondoka nchini Rwanda ndani ya saa 48.

“Serikali ya Rwanda imeijulisha serikali ya Ubelgiji kuhusu uamuzi wake huo wa kuvunja uhusiano wa kidiplomasia haraka, mara moja," imesema wizara ya mambo ya nje ya Rwanda katika taarifa yake jana Jumatatu, ikisisitiza kuwa "uamuzi wa Rwanda umechukuliwa baada ya kuzingatia kwa makini mambo kadhaa, yote yakiwa na uhusiano wa majaribio ya Ubelgiji kuendeleza mambo yake ya ukoloni mamboleo."

Taarifa hiyo imesema mara kwa mara Ubelgiji imekuwa ikiidhoofisha Rwanda, kabla na wakati wa mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao Ubelgiji yenyewe ina mchango wa kina na wa vurugu kihistoria, hasa katika kuchukua hatua dhidi ya Rwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha