Jeshi la Marekani lafanya mashumbulio mapya dhidi ya kundi la Houthi nchini Yemen

(CRI Online) Machi 18, 2025

Jeshi la Marekani limefanya mashambulio mapya ya anga nchini Yemen, likilenga maeneo kadhaa ndani na pembezoni mwa mji wa pwani wa Hodeidah jana jioni.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni kinachoendeshwa na kundi la Houthi, al-Masirah, shambulio moja la angani lililenga eneo la Al-Arj lililoko wilaya ya Bajil, mashariki mwa mji huo, huku mfululizo wa mashambulio mengine ya anga yakilenga na kuharibu kiwanda cha chuma cha Al-Habashi kilichoko wilaya ya Salif, kaskazini magharibi mwa mji huo.

Hakuna ripoti zozote kuhusu vifo ama uharibifu uliotokana na mashambulio hayo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha