China yahimiza G7 kufanya mambo zaidi yanayofaa kwa ushirikiano wa kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2025

BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning amesema China inaitaka G7 kuacha kudhoofisha mamlaka ya China na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, na kufanya mambo zaidi yanayofaa kwa mshikamano na ushirikiano wa kimataifa.

Mao amesema hayo wakati alipotoa maoni juu ya Taarifa ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za G7 na Azimio la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za G7 kuhusu Usalama na Ustawi wa Baharini, ambazo zimetoa kauli za kutowajibika juu ya suala la Taiwan na masuala ya baharini, na kuelezea wasiwasi wao juu ya madai ya China kutoa silaha na bidhaa zenye matumizi mawili kwa Russia, kile kinachoitwa uzalishaji bidhaa kuzidi mahitaji ya soko na upanuzi wa kijeshi wa China, na mambo mengine.

Taarifa hiyo ya pamoja ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za G7 na azimio lao ni upotoshaji wa makusudi wa ukweli na uhalisia wa mambo, ambao una lengo la kuichafua China na kuingilia kati mambo ya ndani ya China, Mao amesema, akibainisha kuwa China inalaani na kupinga vikali jambo hilo na imewasilisha upingaji makini kwa nchi husika.

"Suala la Taiwan ni kiini cha maslahi ya China, ambayo hayakubali kabisa kuingiliwa kati na nje. Hali katika Bahari ya Kusini ya China kwa ujumla ni shwari. Uhuru wa usafiri wa majini na angani katika Bahari ya Kusini ya China haijawahi kuwa suala," amesema Mao, akibainisha G7 inapaswa kuacha kueneza mifarakano na kuzusha mizozo.

China kwa muda wote imekuwa ikihimiza mazungumzo ya amani juu ya suala la Ukraine, haijawahi kutoa silaha hatari kwa upande wowote wa mgogoro huo na imefanya udhibiti mkali juu ya mauzo ya nje ya bidhaa zenye matumizi mawili, amesema, akiongeza kuwa China inakataa kabisa uhamishaji lawama huo wa G7.

Mao amesema, China daima inadumisha vikosi vyake vya nyuklia katika kiwango cha chini kinachohitajika kwa usalama wa taifa, na matumizi kwenye ulinzi ya China ni muhimu ili kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa, ambayo ni ya wazi na yanayofaa.

"Ni viwango viwili wazi wazi kwa G7 kutosema lolote kuhusu wajibu wa Marekani katika kupunguza silaha na hatari za uenezaji nyuklia zinazoletwa na AUKUS, na kuchagua kuelekeza suala hilo kwa China badala yake," Mao amesema.

Kile kinachoitwa "uzalishaji kuliko mahitaji ya soko wa China" kimethibitishwa kuwa uwongo, amesema Mao, akiitaka G7 kuacha kuingiza siasa na kutumia uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kama silaha na kuacha kuharibu utaratibu wa kiuchumi wa kimataifa na kuvuruga utulivu wa minyororo ya viwanda na usambazaji duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha