

Lugha Nyingine
China na Uingereza zaahidi kukabiliana kwa pamoja na mabadiliko ya Tabianchi
Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang akikutana na Ed Miliband, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia Usalama wa Nishati na Utoaji Sifuri wa Nishati Chafuzi mjini Beijing jana Jumatatu. (Xinhua/Ding Haitao)
BEIJING – Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang amekutana na Ed Miliband, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia Usalama wa Nishati na Utoaji Sifuri wa Nishati Chafuzi, mjini Beijing jana Jumatatu, na pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Ding, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuendeleza uhusiano imara na wa kunufaishana kati ya China na Uingereza kunafuatana na maslahi ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili, kuwezesha ukuaji wa uchumi duniani, na kuhimiza juhudi za pamoja za kukabiliana na changamoto za kimataifa.
"China inapenda kushirikiana na Uingereza katika kutekeleza kwa makini maoni muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kuimarisha mwelekeo wa kuboresha na kuendeleza uhusiano wa pande mbili, kuzidisha ushirikiano katika nyanja kama vile huduma za mambo ya fedha, biashara na uwekezaji, na maendeleo yenye kutoa kaboni chache, na kukabiliana na kwa pamoja na mabadiliko ya Tabianchi ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili na dunia," Ding ameongeza.
Kwa upande wake Miliband amesema serikali ya Uingereza inatarajia kwa dhati kuimarisha mawasiliano na China, ina dhamira ya kuendeleza kwa muda mrefu na kiujenzi uhusiano wa pande mbili, na inapenda kuimarisha ushirikiano na China katika kazi za usalama wa nishati na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma