China Bara yaonya adhabu kali kwa washambuliaji mtandaoni wa Taiwan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2025

BEIJING - Msemaji Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, Chen Binhua amesema kuwa Kamandi ya Kikosi cha Habari, Mawasiliano na Elektroniki ya Taiwan (ICEFCOM) imejikadiria kwa kujiweka juu isivyostahili ikifanya mashambulizi ya kimtandao dhidi ya China Bara, akionya kwamba uchochezi huo utakabiliwa na adhabu kali.

Chen amesema hayo jana Jumatatau wakati akijibu swali kutoka kwa vyombo vya habari baada ya Wizara ya Usalama wa Nchi ya China kufichua habari kuhusu watu wanne wa ICEFCOM waliohusika na mashambulizi ya kimtandao dhidi ya China Bara katika makala iliyochapishwa mapema siku hiyo ya Jumatatu.

Chen amesema kuwa kufuatia uchochezi kutoka kwa utawala wa Chama cha Kidemokrasia na Maendeleo (DPP), ICEFCOM inatumika kama mshiriki wa nguvu ya mafarakano ya kutaka “Taiwan ijitenge ” na haiachi juhudi yoyote katika kuanzisha mashambulizi ya kimtandao dhidi ya China Bara au kujaribu kujipenyeza katika China Bara.

Chen ametumai watu wa Taiwan wanaweza kutambua wazi nia ovu na madhara makubwa yanayosababishwa na ufuataji kikaidi wa utawala wa DPP kwa msimamo wao wa kutaka "Taiwan ijitenge", uchochezi wao usiokoma ambao unalenga kutafuta "kujitenga", na vitendo vyao vya kuzidisha mapambano ya kando mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan.

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa watu wa Taiwan kupinga kithabiti aina yoyote ya shughuli za "Taiwan ijitenge", na kulinda kihalisi amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan, vilevile usalama na ustawi wao wenyewe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha