China, Russia na Iran zasisitiza tena mazungumzo ni njia pekee mwafaka kutatua suala la nyuklia la Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Ryabkov Sergey Alexeevich na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Kazem Gharibabadi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 14, 2025. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - China, Russia na Iran zimefanya Mkutano wa Beijing kujadili suala la nyuklia la Iran, katika jitihada mpya za kuimarisha mawasiliano na kuandaa mazingira kwa ajili ya kurejea kwenye mazungumzo ambapo mkutano huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Ma Zhaoxu, kwa kushirikiwa na viongozi wenzake wa Russia na Iran, Ryabkov Sergey Alexeevich na Kazem Gharibabadi.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo siku ya Ijumaa, nchi hizo tatu zimesisitiza juu ya ulazima wa kuoondoa vikwazo vyote visivyo halali vya upande mmoja, na kusisitiza tena kwamba ushiriki wa kisiasa na kidiplomasia na mazungumzo kwa msingi wa kanuni ya kuheshimiana vinabaki kuwa chaguo pekee mwafaka na lenye matokeo.

China na Russia zimekaribisha msisitizo tena wa Iran kwamba mpango wake wa nyuklia ni kwa madhumuni ya amani pekee, na si kwa ajili ya kutengeneza silaha za nyuklia, na pia zimekaribisha dhamira ya Iran ya kufuata kikamilifu wajibu wake chini ya Mkataba wa Kutoeneza Silaha za Nyuklia (NPT) na Makubaliano Jumuishi ya Kulinda, ili kuunga mkono sera ya Iran ya kuendelea kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki na kusisitiza haja ya kuheshimu kikamilifu haki ya Iran ya kutumia nishati ya nyuklia kwa amani kama Nchi Mtia Saini wa NPT.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Ryabkov Sergey Alexeevich na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Kazem Gharibabadi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 14, 2025. (Xinhua/Liu Bin)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Ryabkov Sergey Alexeevich na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Kazem Gharibabadi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 14, 2025. (Xinhua/Liu Bin)

Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), alikutana na wenzake kutoka Russia na Iran ambapo amependekeza kuendelea na dhamira katika mfumo wa Mpango Kazi Jumuishi wa Pamoja (JCPOA) kama msingi wa maafikiano mapya.

"China inatumai kuwa pande zote zitafanya kazi kuelekea mwelekeo sawa na kuanza tena mazungumzo na majadiliano mapema iwezekanavyo. Marekani inapaswa kuonyesha udhati wa kisiasa na kurejea kwenye mazungumzo mapema," Wang amesema.

Amepinga kushinikiza kuingilia kati kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) akisema chini ya hali ya sasa, kuingilia kati haraka kwa UNSC hakutasaidia kujenga imani au kupunguza tofauti kati ya pande husika.

Mkutano huo wa Beijing ni juhudi muhimu za China, Russia na Iran katika kutafuta kusongesha mbele suluhu ya suala la nyuklia la Iran, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha