

Lugha Nyingine
Viongozi waandamizi wa China na Marekani wabadilishana maoni juu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara
He Lifeng, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati Kuu ya Mambo ya Fedha na Uchumi, akikutana na Waziri wa Fedha wa zamani wa Marekani Henry Paulson mjini Beijing, Machi 16, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)
BEIJING - Ofisa Mwandamizi wa China He Lifeng amekutana na Waziri wa zamani wa Fedha wa Marekani Henry Paulson mjini Beijing, na pande hizo mbili zimebadilishana maoni juu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani na uchumi wa dunia.
He Lifeng, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati Kuu ya Mambo ya Fedha na Uchumi, amesema uchumi wa China unadumisha mwelekeo wa ufufukaji, maendeleo ya China yanayosukumwa mbele kwa uvumbuzi yamepata ufanisi dhahiri katika hali ambayo matarajio ya soko yanaendelea kuwa mazuri, na nguvu ya mahitaji ya ndani na nafasi ya mzunguko wa ndani ni kubwa.
"Muundo mpya wa maendeleo ya China unaanzishwa kwa haraka, hali ya kimsingi ya uchumi wa China haijabadilika, na matarajio yake bado ni mazuri,” amesema.
Paulson amesema kuwa uhusiano wa Marekani na China ni muhimu sana na mageuzi ya kijani ni mwelekeo mkuu, Mfuko wa Paulson unapenda kuendelea kufanya juhudi za kuchangia utulivu wa uhusiano kati ya Marekani na China na maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma