China na Laos zaahidi uhusiano imara zaidi kwa mustakabali wa pamoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos Thongsavanh Phomvihane mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 13, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos Thongsavanh Phomvihane mjini Beijing jana Alhamisi, huku viongozi hao wawili wakiahidi kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya China na Laos yenye mustakabali wa pamoja.

Wang ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema katika kipindi cha miaka 64 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, vyama tawala vya China na Laos na mataifa hayo mawili yamekuwa yakisimama pamoja kupitia changamoto na kupeana uungaji mkono. Ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili umekuwa thabiti na himilivu zaidi.”

Wang amesema China inaiunga mkono kithabiti Laos katika kuimarisha uongozi wa chama chake na kueleza nia yake ya kuongeza kuaminiana kimkakati, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Laos yenye mustakabali wa pamoja.

Amebainisha kuwa "Mikutano mikuu miwili" ya China imehitimishwa punde kwa mafanikio, ikiweka lengo la ukuaji wa Pato la Taifa la karibu asilimia 5 kwa mwaka 2025. Amesema, zikiwa makomredi na ndugu, China inaikaribisha Laos kuchangamkia fursa mpya za maendeleo ya China na kushikana mkono kusonga mbele kuelekea maendeleo ya mambo ya kisasa.

Wang amesisitiza kuwa, China iko tayari kufanya kazi na Laos kwa kutilia maanani mwongozo wa kimkakati wa uongozi wa vyama hivyo na nchi hizo mbili, kuimarisha mawasiliano kati ya vyama hivyo na nchi hizo mbili katika ngazi mbalimbali, kuzidisha na kupanua ushirikiano wa kivitendo, kuimarisha ushirikiano wa utekelezaji wa sheria wa pande mbili na wa pande nyingi, na kulinda kwa pamoja amani, utulivu, maendeleo na ustawishaji wa kikanda.

Kwa upande wake Thongsavanh ameipongeza China kwa kufanya kwa mafanikio "mikutano mikuu miwili" na matokeo muhimu, na kusifu maendeleo yenye kupiga hatua kubwa ya China huku kukiwa na mazingira magumu ya nje.

Amesema Laos inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja na iko tayari kufanya kazi na China ili kupiga hatua mkubwa zaidi katika kujenga jumuiya ya Laos na China yenye mustakabali wa pamoja. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos Thongsavanh Phomvihane mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 13, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos Thongsavanh Phomvihane mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 13, 2025. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha