

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa pongezi kwa rais mpya wa Ugiriki Tasoulas kwa kuingia madarakani
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa pongezi kwa rais mpya wa Ugiriki Konstantinos Tasoulas kwa ingia madarakani, akisema kwamba nchi mbili China na Ugiriki zote zina historia ndefu na utamaduni unaong'aa.
Kwenye salamu hiyo ya pongezi iliyotumwa jana Alhamisi, Rais Xi amesema, nchi hizo mbili zimedumisha urafiki wenye kutukuka kwa muda mrefu na ni washirika wa kimkakati wa pande zote wenye kuelewana na ushirikiano wa kuleta manufaa kwa pande zote.
Amesema katika miaka ya hivi karibuni, pande hizo mbili zimeendelea kusukuma mbele mradi wa Bandari ya Piraeus, kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kushirikiana katika kuanzisha Kituo cha Ustaarabu wa Kale wa China na Ugiriki na Shule ya masomo ya fani mbalimbali za zama za kale za China mjini Athens.
“Jitihada kama hizo za pamoja zimeonyesha mapatano ya ustaarabu wa kale wa nchi hizo mbili na hisia zao za uwajibikaji katika dunia ya leo,” Rais Xi amesema.
Amesema kuwa dunia inapitia mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, huku nchi zote zikiwa zimeunganishwa kwa ukaribu na zikikabiliwa na mustakabali wa pamoja, amesisitiza ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote ni njia pekee ya kukabiliana na changamoto za kimataifa.
Rais Xi amesema anaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ugiriki na kupenda kushirikiana na Rais Tasoulas katika kuendelea kuimarisha urafiki wa jadi wa China na Ugiriki, kuongeza ushirikiano wa kunufaishana na mawasiliano ya kitamaduni, kuendelea kuimarisha siku hadi siku hitaji la uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ugiriki, kuhimiza maendeleo endelevu na thabiti ya uhusiano kati ya China na Ulaya, na kuchangia busara na nguvu kwa ajili ya amani, utulivu, maendeleo na ustawi duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma