

Lugha Nyingine
Mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China wamalizika
Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wakihudhuria kwenye mkutano wa tatu wa kufungwa wa Bunge la 14 la Umma la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2025. (Xinhua/Li Xueren)
BEIJING – Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China, ambalo ni chombo kikuu cha utungaji wa sheria cha China umemalizika jana Jumanne, ambapo Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria kwenye mkutano huo wa kufungwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Akiwa amekabidhiwa kazi na Tume ya Utendaji wa mkutano huo, Li Hongzhong, mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo, aliongoza mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe 2,884 wa Bunge hilo.
Wajumbe wameidhinisha ripoti ya kazi ya serikali.
Wamepitisha uamuzi wa kuifanyia marekebisho Sheria kuhusu Wajumbe wa Bunge la Umma la China na wale wa mabunge ya umma ya ngazi mbalimbali. Rais Xi ametia saini amri ya rais kutangaza uamuzi huo.
Watunga sheria wameidhinisha ripoti kuhusu hali ya utekelezaji wa mpango wa mwaka 2024 wa maendeleo ya uchumi na jamii na mswada wa mpango wa mwaka 2025, na kuidhinisha mpango wa mwaka 2025.
Wameidhinisha ripoti kuhusu hali ya utekelezaji wa bajeti ya serikali kuu na ile ya serikali za mitaa kwa mwaka 2024 na mswada wa bajeti ya serikali kuu na ile ya serikali za mitaa kwa mwaka 2025, na kupitisha bajeti ya serikali kuu kwa mwaka 2025.
Pia wameidhinisha ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara Kuu ya Mwendesha Mashtaka ya China.
Akihutubia mkutano huo , Li Hongzhong amehimiza kutekeleza kwa umakini zaidi mipango iliyofanywa kwenye mkutano huo wa Bunge la umma la China na kukamilisha kwa sifa bora malengo na majukumu ya Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2021-2025) chini ya uongozi madhubuti wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiongozi wake.
Li pia ametoa wito wa kutekeleza demokrasia ya umma ya mchakato mzima, kujikita katika kusimamia vyema mambo ya China yenyewe, na kufanya kazi bila kulegalega katika ujenzi wa mambo ya kisasa ya China ulio wa kuhimiza kwa pande zote ustawishaji mkubwa wa Taifa la China.
Kikao cha Tume ya Utendaji na kile cha wenyeviti watendaji wa tume hiyo pia vilifanyika siku hiyo ya Jumanne kabla ya kufungwa kwa mkutano huo wa mwaka wa Bunge la Umma.
Akiwa amekabidhiwa kazi na Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China, Li Hongzhong akiongoza mkutano wa tatu wa kufungwa wa bunge hilo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
Akiwa amekabidhiwa kazi na Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China, Li Hongzhong mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo akiongoza kikao cha nne cha tume hiyo ya utendaji katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
Akiwa amekabidhiwa kazi na Zhao Leji mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendji wa mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China, ambaye ni mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, Li Hongzhong mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo ambaye ni naibu mwenyekiti wa Bunge la Umma la China akiongoza kikao cha tatu cha wenyeviti watendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma