

Lugha Nyingine
China yaonesha msimamo juu ya hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru wa forodha
(CRI Online) Machi 12, 2025
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesisitiza kuwa, China itachukua hatua ya kulipiza kama Marekani itaharibu maslahi yake.
Mao Ning ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali kuhusu Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China na kuuzwa nchini Marekani. Amesema, Marekani imeongeza ushuru wa forodha mara mbili kwa bidhaa zinazotoka China kwa kisingizio cha suala la fentanyl.
Amesisitiza kuwa China kuchukua hatua za kulipiza ni halali na lazima ili kulinda maslahi yake, na kuongeza kuwa, kama Marekani inataka kutatua masuala, inapaswa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili kwa kufanya mazungumzo na China kwa msingi wa usawa, kuheshimiana na kunufaishana.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma