China yaeleza wasiwasi wake juu ya idadi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na mapigano ya kijeshi nchini Syria

(CRI Online) Machi 11, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, China ina wasiwasi mkubwa kutokana na idadi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na mapigano ya kijeshi nchini Syria.

Hivi karibuni, mapigano makali kati ya vikosi vya usalama vya serikali ya mpito ya Syria na vikosi vinavyotii utawala wa zamani wa nchi hiyo yalitokea katika mikoa ya Tartus na Latakia, magharibi ya nchi hiyo, na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi, wakiwemo raia.

Akizungumzia tukio hilo, Mao Ning amesema, China inatoa wito kwa pande husika kusimamisha mara moja mapigano hayo ya kijeshi na vitendo vya uhasama, kulinda usalama wa raia, kuheshimu na kushikilia kanuni ya kuvumiliana, ili kupata mpango wa kujenga upya nchi hiyo unaokidhi matakwa ya watu wa Syria kwa njia ya mazungumzo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha