

Lugha Nyingine
"Taiwan ni mkoa wa China", huu ni msimamo wa siku zote wa Umoja wa Mataifa
BEIJING – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesisitiza jana Jumatatu kuwa, Imeelezwa wazi katika barua ya maoni rasmi ya kisheria ya Ofisi ya Masuala ya Kisheria ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa kwamba "Umoja wa Mataifa unaichukulia 'Taiwan' ni mkoa mmoja wa China usio na hadhi ya kujitenga".
Wakati akijibu swali kuhusu Taiwan kwenye mkutano na waandishi wa habari Machi 7, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alisema kuwa rejeleo pekee la eneo la Taiwan katika Umoja wa Mataifa ni "Taiwan, mkoa wa China."
"Huu ni msimamo wa siku zote wa Umoja wa Mataifa, ambao umewekwa kumbukumbu kwenye nyaraka," Msemaji huyo amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari akijibu swali kuhusu kama taarifa hiyo ya waziri Wang inaonyesha sera kali ya China Bara juu ya Taiwan.
“Azimio namba 2758 lililopitishwa mwaka 1971 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliweka wazi kwamba kuna China moja tu duniani, Taiwan si nchi, na Taiwan ni sehemu moja ya China,” msemaji huyo amesema.
Amesema pia liliweka wazi kuwa kuna kiti kimoja tu cha China katika Umoja wa Mataifa, na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ndiyo mwakilishi pekee katika Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa sheria.
"Umoja wa Mataifa na mashirika yake maalum vinafuata amizio hilo na kuiita Taiwan kuwa ‘Taiwan, mkoa wa China’," msemaji amesema.
Msemaji amesisitiza kuwa, kuhusu suala la Taiwan, msimamo wa China ni wa siku zote na wazi.
"Tunaendelea kuwa na dhamira kwa kanuni ya kuwepo kwa China moja na Makubaliano ya mwaka 1992. Tuko tayari kufanya kazi kwa udhati mkubwa zaidi na kufanya juhudi kubwa ili kufikia muungano kwa amani. Wakati huo huo, China itachukua hatua zote za lazima za kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, na kupinga kithabiti nguvu ya mafarakano ya kuifanya 'Taiwan ijitenge' na uingiliaji kati kutoka nje," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma