Timu ya madaktari wa China yatoa huduma bila malipo mjini Cospicua, Malta

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2025

Madaktari wa Kundi la 20 la timu ya madaktari wa China nchini Malta wakitoa huduma ya ushauri wa kiafya kwa wakazi wenyeji mjini Cospicua, Malta, Machi 9, 2025. (Xinhua/Chen Wenxian)

Madaktari wa Kundi la 20 la timu ya madaktari wa China nchini Malta wakitoa huduma ya ushauri wa kiafya kwa wakazi wenyeji mjini Cospicua, Malta, Machi 9, 2025. (Xinhua/Chen Wenxian)

VALLETTA – Kundi la 20 la timu ya madaktari wa China nchini Malta kutoka Kituo cha Kikanda cha Mediterania cha Tiba ya Jadi ya Kichina (MRCTCM) imetoa huduma za kliniki bila malipo kwa wakaazi wenyeji mjini Cospicua, mashariki mwa Malta, jana Jumapili.

Kwenye shughuli hiyo, timu hiyo ya madaktari ilifanya upimaji wa shinikizo la damu na sukari ya damu, kutoa ushauri mahsusi wa kiafya, na kuchangia vifaa tiba.

Peter Gauci, mkazi mwenyeji mwenye umri wa miaka 89, ameelezea uhitaji wa kujaribu tibabu ya acupuncture ili kupunguza maumivu ya shingo yake. Ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba amekuwa akitumia mafuta ya safflower kwa kutuliza maumivu. "Inanisaidia, na nitaendelea kuitumia," amesema.

Amadeo Brincat, mkazi mwenyeji mwingine mwenye umri wa miaka 33, amewashukuru madaktari hao wa China kwa ushauri wao wa kiafya kuhusu maumivu yake ya mgongo. Ameliambia Xinhua kwamba amekuwa akipata matibabu ya dawa za jadi za Kichina (TCM), ikiwa ni pamoja na acupuncture, mara kadhaa na amepata ahueni kubwa.

Cao Ying (wa kwanza, kulia), daktari wa Kundi la 20 la timu ya madaktari wa China nchini Malta akitoa huduma ya ushauri wa kiafya kwa wakaazi wenyeji mjini Cospicua, Malta, Machi 9, 2025. (Xinhua/Chen Wenxian)

Cao Ying (wa kwanza, kulia), daktari wa Kundi la 20 la timu ya madaktari wa China nchini Malta akitoa huduma ya ushauri wa kiafya kwa wakaazi wenyeji mjini Cospicua, Malta, Machi 9, 2025. (Xinhua/Chen Wenxian)

Makazi mwenyeji Charlo Cutajar, mwenye umri wa miaka 62, ameielezea huduma hiyo ya kliniki bila malipo kama uzoefu "wa ajabu", akielezea urahisi wa kuwa na madaktari wa China wakitoa ushauri wa kiafya umbali wa hatua chache kutoka kwa wakazi. "Ninathamini hilo," amesema.

Akiwa amewahi kufanyiwa tibabu ya acupuncture kwa periarthritis ya bega, alinufaika na uwezo wake wa kutibu vizuri na akaeleza nia ya kujaribu masaji ya jadi ya Kichina ili kupunguza maumivu yake zaidi.

Meya wa Cospicua Marco Agius ameliambia Xinhua kwamba kujitokeza kwa idadi kubwa ya watu kwenye shughuli hiyo kunaonyesha umaarufu wa TCM. "Nina furaha kwamba madaktari wa China wanatoa huduma za kliniki bila malipo kwa jamii yetu," amesema.

Agius, ambaye alipata tibabu ya acupuncture katika MRCTCM mwezi uliopita kwa maumivu ya goti, ameeleza alivyopitia matibabu yake mazuri. "Nilihisi vizuri baada ya matibabu," amesema, akionyesha matumaini kwamba timu hiyo ya madaktari wa China itaendelea kutoa huduma za kliniki bila malipo kwa wakaazi katika siku zijazo.

MRCTCM ilianzishwa na serikali za China na Malta mwaka 1994. Hadi sasa, timu 20 za madaktari wa China zinazojumuisha madaktari zaidi ya 100, zimeshatoa matibabu ya TCM kwa wagonjwa takriban 250,000 wa Malta.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha