Rais Xi asisitiza kuhitimisha kwa mafanikio mpango wa miaka mitano wa maendeleo ya jeshi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2025

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihudhuria kikao cha wajumbe wote wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 2025, 2027. (Xinhua/Li Genge)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihudhuria kikao cha wajumbe wote wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Machi 2025, 2027. (Xinhua/Li Genge)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Ijumaa alipokuwa akihudhuria kikao cha wajumbe wote wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China katika mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, unaoendelea mjini Beijing, mji mkuu wa China, amesisitiza kuhitimisha kwa mafanikio Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya jeshi (2021-2025).

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesema ni lazima kuimarisha kujiamini, kukabiliana na changamoto ana kwa ana, na kutekeleza matakwa kwa maendeleo bora ya hali ya juu ili kutimiza malengo na majukumu yaliyowekwa kwa wakati uliopangwa.

“Katika kipindi cha miaka minne na zaidi iliyopita tangu kutekelezwa kwa mpango huo, mafanikio makubwa yamefikiwa, wakati huohuo pia kuna changamoto na masuala mengi yanayohitaji kushughulikiwa,” amesema.

Rais Xi amesisitiza kufuata njia ya maendeleo ya kijeshi yenye ubora, ufanisi mkubwa, gharama nafuu na uendelevu ili kuhakikisha kwamba matokeo yake yanastahimili majaribu ya wakati na mapigano halisi.

Amesisitiza umuhimu wa kutumia dhana na mbinu za kisasa za usimamizi, na kuboresha kila mara mifumo na taratibu za usimamizi wa kimkakati ili kutekeleza mpango huo kwa namna ya kitaratibu, kikamilifu na iliyoratibiwa zaidi.

Akisisitiza kuongeza bidii za pamoja za kijeshi za kiraia, na juhudi za kutumia vyema nguvu na rasilimali za sekta za kiraia ili kuongeza ubora na ufanisi wa maendeleo ya jeshi.

Akitoa wito wa kuharakishwa maendeleo ya nguvu bora za kupambana zenye sifa mpya, Rais Xi amehimiza juhudi za kuboresha mfumo wa mwitikio wa kasi na mageuzi ya haraka ya teknolojia mpya.

Pia ametaka kuanzisha mfumo mzuri na madhubuti wa uangalizi ili kuchunguza kwa kina na kushughulikia ufisadi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha