

Lugha Nyingine
Xi Jinping asisitiza umuhimu wa elimu katika kuunga mkono maendeleo ya sayansi na teknolojia na kuandaa vipaji
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwatembelea washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka vyama vya kidemokrasia vya China vya Shirikisho la Demokrasia la China na Shirikisho la Uhimizaji wa Demokrasia la China, na sekta ya elimu, ambao wanahudhuria mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China mjini Beijing, Machi 6, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza kuimarisha umuhimu wa elimu katika kuunga mkono maendeleo ya sayansi na teknolojia na kuandaa vipaji, akitoa wito wa kuelewa kwa kina mahitaji ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China kwa elimu, sayansi na teknolojia, na vipaji.
"Lengo ni kuwaandaa watu wenye ujuzi na vipaji wengi zaidi siku hadi siku, kuwawezesha waoneshe vilivyo uwezo wao, na kuhakikisha uwezo wao unatumiwa kikamilifu," Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesema Alhamisi wakati akihudhuria kikao cha pamoja cha kikundi cha wajumbe kwenye mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC).
Kikao hicho kilihudhuriwa na washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka Vyama vya Kidemokrasia vya China vya Shirikisho la Demokrasia la China, na Shirikisho la Uhimizaji wa Demokrasia la China, pamoja na waliotoka sekta ya elimu.
Rais Xi amesisitiza ni lazima kushikilia mwelekeo sahihi wa uendeshaji wa shule kwenye mchakato wa kujenga China kuwa nchi inayoongoza katika elimu, sayansi na teknolojia, na vipaji.
Ametoa wito wa kuwaandaa vijana wa kizazi kipya wenye uwezo na msingi wa kufuata maadili, uwezo wa kiweledi, afya nzuri, hali bora ya kihisia, na ustadi wa kazi za ufundi unaohitajika kwa kujiunga na kuendeleza mambo ya kijamaa.
Amesisitiza kuwa ni lazima kuwafanya wanafunzi wawe na Fikra juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya.
Rais Xi amesema "Ili kujenga mfumo wa elimu wa sifa bora unaokidhi matarajio ya watu, umuhimu mkubwa ni kuendeleza mageuzi ya kina ya elimu," ni muhimu kuboresha mfumo wa usimamizi wa shule, kuzipa shule haki ya kujiamulia kazi zake, na kuhimiza siku hadi siku usimamizi wa shule unaofanyika kwa mujibu wa sheria.
"Ili kufikia mchangamano mzuri kati ya uvumbuzi wa kujitegemea wa kisayansi na kiteknolojia na kuwaandaa vipaji wenye uwezo mkubwa, ni lazima kuifanya elimu ioneshe zaidi umuhimu wake wa kuongoza wa kimsingi katika kuunga mkono uvumbizi wa kiteknolojia na kuwaandaa vipaji" Rais Xi amesema.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwatembelea washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka Vyama vya Kidemokrasia vya China vya Shirikisho la Demokrasia la China, na Shirikisho la Uhimizaji wa Demokrasia la China, pamoja na sekta ya elimu, ambao wanahudhuria mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China mjini Beijing, Machi 6, 2025. (Sheng Jiapeng/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China, akiwatembelea washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka vyama vya kidemokrasia vya China, na sekta ya elimu, ambao wanahudhuria mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China mjini Beijing, Machi 6, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
Rais Xi Jinping wa China, akiwatembelea washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka vyama vya kidemokrasia vya China, na sekta ya elimu, ambao wanahudhuria mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China mjini Beijing, Machi 6, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma