Rais Xi wa China ahimiza Mkoa wa Jiangsu kufanya kazi kubwa katika maendeleo ya nchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2025

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika kikao cha mashauriano na majadiliano na wajumbe kutoka Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China unaofanyika Beijing, mji mkuu wa China, Machi 5, 2025. (Picha na Zhan Zheng/Xinhua)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, siku ya Jumatano wakati akishiriki katika kikao cha mashauriano na majadiliano na wajumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China unaofanyika Beijing, amehimiza Mkoa huo wa Jiangsu, mashariki mwa China, ambao ni mkoa wenye nguvu kubwa ya kiuchumi, kufanya kazi kubwa katika maendeleo ya jumla ya nchi ya China.

Rais Xi amesema, “Jiangsu inapaswa kutangulia mbele katika kufungamanisha uvumbuzi wa teknolojia na kazi za viwanda, kuhimiza mageuzi ya kina na ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kutekeleza mikakati mikuu ya maendeleo ya nchi,” na mkoa huo unapaswa kuweka mfano katika kutafuta ustawi wa pamoja.

Baada ya kusikiliza hotuba zilizotolewa na wajumbe kadhaa wanaohudhuria Mkutano wa tatu wa Bunge hilo la 14, Rais Xi amesema uvumbuzi wa teknolojia na wa kazi za viwanda ni njia ya kimsingi ya kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.

Rais Xi amesema, “Ili kuhimiza uvumbuzi wa teknolojia, ni muhimu kuufanya mfumo wa viwanda kuwa wa mambo ya kisasa na kufanya mpango wa jumla kuhusu elimu, sayansi na teknolojia, na ukuzaji vipaji,” ili kuhimiza kazi za kuyabadilisha matokeo mengi zaidi ya kisayansi na kiteknolojia kuwa nguvu halisi za uzalishaji.

Rais Xi ameutaka mkoa huo kuendeleza kwa kina mageuzi na ufunguaji mlango, kufanya mipango ya jumla kuhusu matakwa ya ndani na kimataifa, kufungamanisha vizuri kazi za mijini na vijijini, kuyafanya maeneo yote kushirikiana katika kazi zote, kuboresha mpangilio wa nguvu za uzalishaji, na kutoa nguvu zaidi katika kuhimiza maendeleo ya sifa bora ya hali ya juu.

Ameongeza kuwa utendeaji kwa usawa lazima uhakikishwe kwa kampuni na viwanda vya umilikaji wa aina mbalimbali, na ni lazima kuendelea na juhudi za kuboresha mazingira ya biashara.

Rais Xi amehimiza mkoa huo kufanya juhudi za kujitokeza, na maeneo yote ya mkoa huo kushirikiana pamoja katika utekelezaji wa mikakati ya maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Changjiang , maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Changjiang.

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika kikao cha mashauriano na majadiliano na wajumbe kutoka Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 5, 2025. (Picha na Sheng Jiapeng /Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika kikao cha mashauriano na majadiliano na wajumbe kutoka Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 5, 2025. (Xinhua/Yan Yan)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha