Uzuri wa Majira: Kuamka kwa Wadudu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2025

Habari, kila mmoja! Mpenda kusafiri, Sisi hapa! Leo ni Jingzhe, au kuamka kwa wadudu, kipindi katika vipindi 24 vya hali ya hewa kwa kalenda ya kilimo ya China ambapo vitu vyote hukua kwa hali motomoto. Hebu twende Wilaya ya Wuyuan ya Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China kuangalia hali halisi huko!

Mlio wa radi unaunguruma, na majira ya mchipuko yanapumua uhai kwenye ardhi yote. Jingzhe, katika lugha ya Kichina, inamaanisha miungurumo ya radi, ikiamsha viumbe vilivyo lala nusu kaputi. Kwa sasa, mashamba ya Wuyuan pia yametapakaa maisha ya viumbe. Mashamba ya kwenye miteremko ya milima yamegeuka kuwa bahari za dhahabu za maua ya rapa, huku maua ya matunda ya mapichi na maplamu yakichanua kushindana kwa mvuto. Mlipuko wa maua hayo na majengo yenye mtindo wa kienyeji wa Kabila la Wahui vinaongezeana uzuri wao, vikiunda mandhari ya majira ya mchipuko yaliyojaa uhai na furaha.

Mimea pori ni ladha bora kwa majira ya mchipuko wilayani Wuyuan. Katika kipindi hiki cha Jingzhe, mimea pori katika Kijiji cha Sixiyan inastawi. Milipuko ya ladha kama vile “Majani ya Malantou” na “Fish Mint” tayari imeanza kujaza meza za chakula za wenyeji!

Kipindi hiki cha Jingzhe pia kinamaanisha ni wakati kwa wakulima kuanza kufanya kazi! Katika Mji wa Wuyuan na sehemu nyingi nchini China, kazi ya kilimo huanza kwa kasi kwenye kipindi hiki. Baada ya majira mazima ya baridi ya kupumzika, nguvu ya mazingira ya asili inaamka kimyakimya!

“Ngurumo ya Majira ya mchipuko inaashiria ufufukaji mkubwa wa viumbe vya asili.” Mwezi Machi unapofika kineema, ninatuma mwangwi wa ngurumo ya majira haya ya mchimpuko kwa nyie marafiki zangu mliopo mbali. Uzuri wote uliokuwa umelala nusu kaputi sasa unaamka hapa China, je, ni kitu gani kinachanua katika sehemu yako ya Dunia?

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha