

Lugha Nyingine
Trump asema asilimia 25 ya ushuru kwa Mexico na Canada kuanza kutozwa "leo"
Rais wa Marekani Donald Trump akihudhuria mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington D.C., Marekani, Februari 13, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)
WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatatu kwamba asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada itaanza kutozwa rasmi leo Jumanne, Machi 4.
"Muhimu sana, kesho (leo Jumanne), ushuru, asilimia 25 kwa Canada na asilimia 25 kwa Mexico, na hiyo itaanza," Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House.
"Kile wanachopaswa kufanya ni kujenga viwanda vyao vya magari, kiukweli, na vitu vingine nchini Marekani, katika mazingira ambayo hawatatozwa ushuru," Trump amesema.
Trump pia amesisitiza kwamba ushuru wa kutozana kwa usawa utaanza Aprili 2.
Februari 1, Trump alitia saini amri tendaji ya kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa Marekani kutoka Mexico na Canada, huku kukiwa na ongezeko la ushuru wa asilimia 10 mahsusi kwa bidhaa za nishati za Canada.
Februari 3, Trump alitangaza kwamba ushuru huo wa ziada kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada utaahirishwa kwa mwezi mmoja, kuruhusu muda zaidi wa majadiliano.
Kwa mujibu wa uamuzi huo, hatua husika za ushuru zimepangwa kuanza kutumika leo Machi 4.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma