

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa Uingereza atangaza mpango mpya wa pauni 1.6 bilioni kwa Ukraine kununua makombora
Picha hii iliyopigwa Agosti 15, 2024 ikionyesha kifaru cha kivita cha Ukraine kilichoharibiwa katika mashambulizi ya Russia mjini Toretsk. (Picha na Peter Druk/Xinhua)
LONDON - Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ametangaza jana Jumapili kwamba Uingereza itairuhusu Ukraine kutumia pauni bilioni 1.6 (dola bilioni 2 za Kimarekani) za fedha za mauzo ya nje ya Uingereza kununua makombora zaidi ya 5,000 ya ulinzi wa anga akisema: "Hii itakuwa muhimu kwa kulinda miundombinu muhimu na kuiimarisha Ukraine".
Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa kilele na viongozi wa nchi za Magharibi jijini London, Starmer ameongeza kuwa, lengo ni "kuiweka Ukraine katika nafasi yenye nguvu zaidi" ili nchi hiyo iweze kujadiliana kutoka katika nafasi ya nguvu”.
Viongozi wa nchi za Magharibi, wakiwemo wakuu wa nchi kadhaa wa Ulaya na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, walikusanyika London Jumapili kwa mkutano huo wa kilele wa ulinzi uliolenga kusongesha mbele mpango wa amani kwa Ukraine.
Starmer amesema viongozi katika mkutano huo wamekubaliana juu ya mpango wenye hatua nne kuhakikisha amani nchini Ukraine: kudumisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine wakati mgogoro ukiendelea na kuongeza shinikizo la kiuchumi kwa Russia; kuhakikisha kwamba amani yoyote ya kudumu inahakikisha mamlaka na ulinzi wa Ukraine, huku Ukraine ikiwa mezani kwa kila majadiliano; kuzuia "uvamizi wowote wa baadaye wa Russia" katika tukio la makubaliano ya amani; na kuanzisha "muungano wa uhiari" kuilinda Ukraine na kudumisha amani nchini humo.
Bendera za Umoja wa Ulaya (EU) na Ukraine zikionekana kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Februari 24, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
Viongozi hao pia wamekubaliana kukutana tena hivi karibuni ili kuendeleza kasi ya juhudi hizo, Starmer amesema.
Waziri Mkuu huyo amesisitiza tena dhamira ya Uingereza kuunga mkono mpango huo wa amani kwa "buti ardhini, na ndege angani."
"Ulaya lazima ifanye ubebaji mzigo mzito," amesema, akisisitiza kwamba makubaliano hayo yanahitaji uungwaji mkono wa Marekani.
Mapema siku hiyo Jumapili kabla ya mkutano huo, Starmer alitangaza kuwa Uingereza, Ufaransa na Ukraine zitafanyia kazi mpango wa kusimamisha mapigano utakaowasilishwa kwa Marekani. Alitaja mambo matatu muhimu ili kufikia "amani ya kudumu" -- Ukraine yenye nguvu, kipengele cha Ulaya yenye dhamana ya usalama, na kizuizi cha nyuma cha Marekani, huku jambo hilo la mwisho likiwa mada ya "majadiliano" makali.
Mkutano huo umefanyika huku kukiwa na mvutano wa kidiplomasia, kufuatia majibizano makali mapema wiki hii kati ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House, ambayo yalisababisha kufutwa kwa makubaliano yaliyotarajiwa ya malighafi kati ya nchi hizo mbili.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (Kulia) akipeana mkono na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mbele ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mtaa Na. 10 wa Downing jijini London, Uingereza, Machi 1, 2025.(Xinhua/Li Ying)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma