

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Sergei Shoigu, katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Februari 28, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Sergei Shoigu, katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, Ijumaa mjini Beijing akisema kuwa China na Russia ni majirani wa kirafiki na marafiki wa kweli, na kwamba yeye na Rais Vladimir Putin wamewasiliana mara mbili hadi sasa mwaka huu, wakipanga mipango mikubwa ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia na kuwa na mazungumzo ya kina kuhusu masuala makubwa mbalimbali ya kimataifa na kikanda.
Amesema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa Vita vilivyofanywa Watu wa China vya kupambana na Uvamizi wa Japan, Vita Kuu vya Kulinda Nchi vya Umoja wa Kisovieti na Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, pamoja na maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.
"Katika mwaka huu wenye umuhimu maalum wa kihistoria, uhusiano kati ya China na Russia utakumbatia mfululizo wa ajenda muhimu," Rais Xi amesema.
Amesema pande hizo mbili zinapaswa kudumisha mawasiliano ya karibu kwenye ngazi zote ili kutekeleza kikamilifu makubaliano yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili na kuhimiza ujirani mwema na urafiki wa kudumu, uratibu wa kimkakati wa pande zote na ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.
Ametoa wito kwa pande zote mbili kuzidisha kila wakati uratibu wa kimkakati na ushirikiano wa manufaa halisi ili kuchangia maendeleo ya pamoja na ustawishaji wa nchi hizo mbili.
"Pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kuimarisha uratibu katika masuala ya kimataifa na kikanda, kutoa mchango kamili kwa nchi za BRICS na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, na kusaidia kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya Nchi za Kusini," Rais Xi amesema.
Kwa upande wake Shoigu amewasilisha salamu za Rais Putin kwa Rais Xi, akisema kuwa Rais Putin anathamini sana urafiki wa dhati na mawasiliano ya karibu na Rais Xi.
"Uhusiano kati ya Russia na China umefikia ngazi ya juu ambayo haijawahi kutokea na haulengi upande wowote wa tatu," Shoigu amesema.
Amesema Russia inathamini sana juhudi za China za kila wakati kuhimiza utatuzi wa amani wa mgogoro wa Ukraine.
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Sergei Shoigu, katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Februari 28, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma