Nchi za Ulaya zaapa kulipiza kisasi dhidi ya tishio la ushuru la Trump

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2025

Bendera za Umoja wa Ulaya zikipepea nje ya Jengo la Berlaymont, makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji, Januari 29, 2025. (Xinhua/Meng Dingbo)

Bendera za Umoja wa Ulaya zikipepea nje ya Jengo la Berlaymont, makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji, Januari 29, 2025. (Xinhua/Meng Dingbo)

BRUSSELS -Mvutano wa kibiashara katika pande za Bahari ya Atlantiki za Marekani na nchi za Ulaya umeongezeka baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za Ulaya zinazoingia nchini humo, huku nchi za Ulaya zikionya kuwa Ulaya itajibu "kithabiti na mara moja" dhidi ya vikwazo hivyo visivyo na msingi.

Mpango huo wa ushuru uliotangazwa na Trump siku ya Jumatano wiki hii unagusa bidhaa za Ulaya kwenye soko la Marekani, yakiwemo magari na bidhaa nyingine. Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la mawaziri katika Ikulu ya White House, Trump amedai kuwa EU "imekuwa ikiitumia" Marekani kwa kuzuia magari na bidhaa za kilimo za Marekani.

Akijibu madai hayo, msemaji wa Kamisheni ya Ulaya Olof Gill amesema Alhamisi kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba biashara za Marekani zimekuwa zikipata faida kubwa kutoka kwenye uwekezaji barani Ulaya.

"Kwa kuunda soko moja kubwa na jumuishi, Umoja wa Ulaya (EU) umewezesha biashara, kupunguza gharama kwa wauzaji nje bidhaa wa EU na kusawazisha viwango na kanuni katika nchi zote wanachama wetu. Kwa sababu hiyo, uwekezaji wa Marekani barani Ulaya una faida kubwa," amesisitiza.

Kuhusu ushuru huo, Kamisheni ya Ulaya ilisema mapema Jumatano kwamba EU itajibu "kithabiti na mara moja" dhidi ya vizuizi visivyo vya haki kwa biashara huria na yenye usawa, ikiwemo wakati ushuru unapotumiwa kupinga sera za kisheria na zisizo za kibaguzi.

Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola akihudhuria mkutano maalum wa Baraza la Ulaya kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Mei 30, 2022. (Xinhua/Zheng Huansong)

Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola akihudhuria mkutano maalum wa Baraza la Ulaya kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji, Mei 30, 2022. (Xinhua/Zheng Huansong)

Akizungumza mjini Washington siku jana Alhamisi, Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola amesisitiza kwamba Ulaya na Marekani zina maadili sawasawa na kuonya dhidi ya kujitenga. Amesisitiza tena kwamba EU iko tayari kujibu "kithabiti na mara moja dhidi ya vizuizi visivyo vya haki kwa biashara huria na ya usawa."

Nchi nyingine za Ulaya zikiwemo Ufaransa na Hispania zinachangia msimamo huo wa EU juu ya kulipiza kisasi, zikitoa wito wa umoja kutetea maslahi ya Ulaya.

"Tunahitaji kuwa na majibu thabiti na sawia," Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu ameiambia Radio ya Ufaransa, France Info katika mahojiano siku ya Alhamisi.

Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) akipeana mkono na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Februari 24, 2025. Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumatatu kwamba ushuru kwa Mexico na Canada "utasonga mbele." (Xinhua/Hu Yousong)

EU itajilinda "dhidi ya wale wanaoishambulia kwa ushuru usio na msingi ambao unatishia mamlaka yetu ya kiuchumi," Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez amesema kwenye hafla iliyofanyika Mkoa wa Basque kaskazini mwa Hispania.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha