Xi asisitiza wajibu na hatua mpya katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2025

BEIJING – Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amewataka maofisa waandamizi wa chama kubeba wajibu mpya na kuchukua hatua mpya kwa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.

Xi amesema hayo baada ya kusoma ripoti za kazi za mwaka za viongozi waandamizi wa Chama zilizowasilishwa hivi karibuni kwa Kamati Kuu ya Chama na Katibu Mkuu wake.

Maofisa hao ni pamoja na wajumbe wa Ofisi ya Siasa na Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama, na wajumbe viongozi wa vikundi vya uongozi vya Chama vya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, pamoja na makatibu wa vikundi vya uongozi vya Chama vya Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya Umma ya China.

Xi amedhihirisha kuwa, mwaka huu ni wa mwisho wa utekelezaji wa Mpango wa 14 wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021-2025) na pia ni mwaka muhimu wa kuendeleza mageuzi kwa kina zaidi kwa pande zote, ambapo majukumu ni magumu katika kuhimiza mageuzi na maendeleo na kudumisha utulivu.

Rais huyo pia amehimiza kutekeleza kithabiti sera na maamuzi makuu ya Kamati Kuu ya Chama na kufikia malengo yaliyowekwa katika Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano kwa sifa bora ili kuweka msingi imara kwa mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2026-2030).

Rais Xi pia amewataka maofisa viongozi kuwa na utulivu wakati wa kukabiliana na changamoto zozote zinazotokana na mabadiliko ya hali ya ndani na nje ya nchi, kuharakisha kujenga muundo mpya wa maendeleo, kuendeleza mageuzi kwa kina na kwa pande zote, kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kuhimiza uchumi uendelee kufufuka vizuri na kupata ongezeko siku hadi siku.

Xi pia amewataka maofisa viongozi kuimarisha kazi ya kufanya utafiti na kujifunza, kufuata kwa umakini maamuzi manane ya Kamati Kuu ya Chama kuhusu kurekebisha mienendo, na kutimiza kwa hiari wajibu wa kisiasa wa Chama kujiendesha kwa nidhamu kali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha