China yapinga Canada kuziwekea vikwazo kampuni za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2025

BEIJING – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lin Jian amesema kitendo cha Canada cha kuziwekea vikwazo kampuni za China ni kitendo kisicho cha halali na pia ni cha makosa.

"China inakipinga kwa uthabiti na imewasilisha malalamiko mazito kwa upande wa Canada," Lin amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu alipoulizwa kuhusu Canada kutangaza kuweka vikwazo kwa kampuni na watu binafsi wa kigeni 76 kwa kutoa bidhaa za matumizi ya kijeshi na kiraia kwa Russia, zikiwemo kampuni zaidi ya 20 za China.

"China daima inapinga vikwazo vya upande mmoja ambavyo havina msingi wa sheria ya kimataifa na havijathibitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa," Lin ameongeza.

"China siku zote inafuata msimamo wa kutetea haki kwa kufuata hali halisi juu ya suala la Ukraine," Lin amesema, akiongeza kuwa China inafanya juhudi zaidi za kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa msukosuko, haikutoa silaha za mauaji kwa pande zinazopigana, ikidhibiti kwa umakini uuzaji nje wa bidhaa zenye matumizi ya kijeshi na kiraia, na wigo na hatua zake za udhibiti wa uuzaji nje wa droni ni kali zaidi duniani.

"Kama zilivyofanya nchi nyingine, China inafanya ushirikiano wa kawaida wa kiuchumi na kibiashara na Russia kwenye msingi wa kuwa na usawa na kunufaishana, hili ni jambo halali na halipingiki " Lin amesema.

“China inahimiza Canada kubatilisha mara moja uamuzi wake huo wa makosa. China itachukua hatua za lazima ili kulinda kwa uthabiti haki na maslahi halali ya kampuni za China,” Lin ameongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha