

Lugha Nyingine
Trump asema ushuru kwa Mexico, Canada "kuendelea"
Rais Donald Trump wa Marekani akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (hayupo pichani) katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Februari 24, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)
WASHINGTON - Rais Donald Trump wa Marekani jana Jumatatu alipoulizwa kuhusu muda wa mwisho wa kuanza kutoza ushuru kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya White House kwamba "ushuru unaendelea."
"Tuko katika wakati na ushuru, na inaonekana kama inakwenda haraka sana," Trump amesema, akiongeza kuwa, "Sasa ushuru unaendelea, kwa wakati, katika ratiba."
Trump amedai tena kwamba "tumekuwa tukitendewa vibaya sana na nchi nyingi, si tu Canada na Mexico. Tumetumiwa vibaya."
"Kile tunachotaka ni kunufaishana. Tunataka kutendeana kwa usawa. Tunataka kuwa na mambo sawa, kwa hivyo kama kuna mtu atatutoza, tunamtoza," Trump amesema.
Februari 1, Trump alitia saini amri tendaji ya kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Mexico na Canada, huku kukiwa na ongezeko la ushuru wa asilimia 10 mahsusi kwa bidhaa za nishati za Canada.
Februari 3, Trump alitangaza kwamba ongezeko hilo la ushuru kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada litaahirishwa kwa mwezi mmoja, kuruhusu muda zaidi wa majadiliano.
Rais Donald Trump wa Marekani na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wakihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Februari 24, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma