China yasisitiza tena dhamira kwa ushirikiano wa kimataifa katika haki za binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 25, 2025

Chinese Foreign Minister Wang Yi, also a member of the Political Bureau of the Communist Party of China Central Committee, delivers a video address at the high-level meeting of the 58th session of the United Nations Human Rights Council, Feb. 24, 2025. (Xinhua/Lian Yi)

Wang Yi, waziri wa mambo ya nje wa China akihutubia kupitia video kikao cha ngazi ya juu cha mkutano wa 58 wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa Februari 24, 2025. (Xinhua/Lian Yi)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye kikao cha ngazi ya juu cha mkutano wa 58 wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu, akisisitiza nia ya China ya kushirikiana na nchi zote kushikilia mtazamo sahihi wa haki za binadamu na kusukuma mageuzi na maboresho ya usimamizi bora wa haki za binadamu duniani.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema ni muhimu kukumbuka dhamira ya awali ya usimamizi wa haki za binadamu, ambayo inatilia maanani watu.

Amesisitiza kuwa, China inakataa kithabiti vitendo vinavyoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha haki za binadamu na kupuuza mamlaka ya nchi, ulinzi na usalama wa maisha ya watu.

"Haki na usawa lazima vidumishwe, na haki ya kujikimu na maendeleo zinapaswa kupewa kipaumbele kama haki za kimsingi za binadamu," Wang amesema, akiongeza kuwa viwango viwili au hata viwango vingi katika masuala ya haki za binadamu lazima vikataliwe vikali.

"Lazima kusisitiza mawasiliano na kufunzana. Lazima pia tukatae kwa uthabiti vitendo au kauli zozote zinazotaka kulazimisha nchi nyingine kufuata mifano na mapendeleo ya nchi binafsi, au kuingiza mambo ya siasa, kutumia vibaya na kugeuza haki za binadamu kuwa silaha," Wang ameongeza.

Wang amesema China inapenda kushirikiana na nchi nyingine ili kufikia dunia ya mambo ya kisasa yenye sifa ya maendeleo ya amani, ushirikiano wa kunufaishana, na kustawishwa pamoja.

“China inafanya juhudi kwa mustakabali na ustawi wa binadamu na nchi zote. Itahimiza ushirikiano wa kimataifa na mawasiliano ya ustaarabu na kuwa mjenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, huku ikijihusisha kikamilifu zaidi katika ushirikiano wa kimataifa wa haki za binadamu ili kujenga mustakabali mwema wa haki za binadamu duniani kote,” Wang ameongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha